Na Geofrey Stephen Arusha
Kanisa la kilutheri Afrika Mashariki(KKAM) limewasimika na kuwaingiza kazini watumishi wawili amabo ni mchungaji Dr Philemon Langas Molel kuwa Askofu wa Jimbo la Arusha Mashariki pamoja na mch Dr Philemon Olaisi Molel (MONABAN) kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Hilo .
Askofu mkuu wa kanisa Hilo Askofu Osca John Olotu akizungumza katika ibada ya kuwasimika watumishi hao ;iliyofanyika maeneo ya Ngulelo ,amesema kuwa wametimiza agizo la Mungu aliloagiza la enendeni ulimwenguni mkahubiri Injili.
Amesema kuwa ili kusudi Hilo litimie lazima wahubiri Injili kupitia utumishi waliopewa hivyo kupitia watumishi hao wanatarajia waumini kuongezeka na wanatarajia kufikia vijiji vyote ili kupeleka Injili.
Ameongeza kuwa wao hawatafanya mashindano ya aina yeyote badala yake watasimamia kusudi moja la kuhubiri Injili ya Yesu Kristo.
Akizungumza Mara baada ya kuingizwa rasmi kazini Askofu Dr Philemon Langas Molel amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa daraja jipya alilolipokea na wajibu walio nao ni kuhakikisha wanaotesha makanisa sehemu mbali mbali.
Ameongeza kuwa kanisa Hilo na mengine hayana tofauti kwani yote yanalenga kumhubiri Yesu Kristo lakini tofauti ndogo ikiwa ni kutowabariki wanawake kuwa wachungaji.
Kwa upande wake msaidizi wa Askofu mchungaji Dr Philemon Olaisi Molel (MONABAN)akiongea Mara baada ya kubarikiwa na kuingizwa kazini amesema kuwa amesikia furaha Sana kwani kanisa Hilo linahubiri Amani na ushirikiano
‘Kanisa letu tutakuwa tunahubiri upendo Amani, ushirikiano na umoja katika maeneo yote nchini na hata kwenye nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.”ameisisitizia Monaban
Monaban Amedai kuwa kwa kuwa Mungu amempa vipawa viwili ikiwemo Cha Siasa pamoja na utumishi wa madhabauni atavitumia vyote kwa pamoja kwa kuwa atawahidumia watu wake kiroho na kimwili na atahakikisha anavitumia vizuri Kama Mungu alivyokusudia.
Katibu wa kanisa Hilo Afrika Mashariki Heroki Mkwizu amesema kuwa parokia nyingi kwa Sasa zitafunguliwa Arusha pamoja na maeneo mengine Mara baada ya kuongezeka kwa watumishi hao
Mwisho