Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Gilbert Kalima Amewataka wale wote wenye sifa za kugombea kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na kuacha kuendelea kutumiwa Kwa maslahi ya viongozi wachache wanaotaka madaraka.
Aidha ameeleza kwamba viongozi wapya wa matawi wa Jumuiya hiyo tunataka kuona jumuiya ikimarika kiuchumi kwa kila mkoa kuhakikisha iongoze na ijipange kuimarika kiuchumi.
Kalima Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na viongozi wa Baraza kuu la mkoa wa Arusha katika ukumbi wa CCM mkoa Jijini Arusha ambao aliitaka Jumuiya ya Wazazi kuwa ya mfano kwa tuwe uadilifu na wmfano kwa Jumuiya zengine katika kukiimarisha chama na kujenga Utulivu kwa kuimarisha Amani miongozo na kanuni sanjari na kujiimarisha uchumi.
Watu wanaenda kushawishiwa anayeshawishiwa Kwa maslahi ya mtu ajitafakari au yule anayeambiwa akachukuwe fomu ujue amefilisika na ajiulize mara mbili kama anafaa kwa nafasi hiyo kwani huu sio muda wa kuwabeba watu wasiotufaa.
“Sisi viongozi wa Jumuiya na chama tuwe wa mfano Arusha na idhihirishe kuwa Jumuiya hii ni ya mfano kwa kujenga uchumi ndani ya Jumuiya kuifanya kuimarika kiuchumi kuendana na Msingi ya kuigwa na Jumuiya zengine”
Tukienda kwenye ahadi tulizitoa kwa wananchi inakaiwa Jumuiya kukaa na kuona serikali inatekeleza ilani tukianza kulaumiana sisi kwa sisi hilo sio Lengo la chama chetu.
Tuhakikishe tunaulizia na kufuatilia Ilani ya uchaguzi kukagua na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ili kujua Yale tulioahidi yamefanyika ili tuendelee kushuka dola.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen Amewataka Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kamamieni kanuni na miongozo katika kukisimamia Chama kwa utaratibu wa vikao na sio kwenye mitandao.
Amewataka watumie mitandao kujenga chama na Jumuiya zake na tuache kuweka Siri zetu mitandaoni za kukibomoa chama chetu kwani sisi nyie dira ya utendaji na Msingi wa mafanikio yaliopo
“Msingi Mkubwa uwe ni kukiimarisha chama na sio vingine Jumuiya ya Wazazi ipo salama haina makando kando naziomba Jumuiya zengine pamoja na chama kuiga mfano huu”