Site icon A24TV News

LUSHOTO YANG’ARA MIRADI YA MAJI MWENGE WAZINDUA,MBUNGE AMFAGILIA DC KALISTI USIMAMIZI MIRADI

Fedha za Mapango wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhiki ya Uviko 19 zaidi ya shilingi milioni 782.5 zimeweza kuwanufaisha wakazi zaidi ya 11,048 kupata maji Safi na salama katika vijiji 11 vya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.
Hayo yalisemwa Jana na Kaimu Meneja  wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Tanga(RUWASA),Injinia Erwin Sizinga mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa,Sahili Geraruma muda mfupi kabla ya kuzindua miradi hiyo katika Halmashauri ya Bumbuli na Halmashauri ya Lushoto.
Injinia Sizinga alisema fedha za Uviko 19 zilisaidia kupata Mkandarasi kampuni ya Mbesso Construction ya Jijini Dar es Salaam ambaye alisema kuwa mradi huo wa maji utasaidia kujenga mradi wa maji ambao utasaidia upatikanaji wa maji katika vijiji viwili vya Mayo na Kizinda vilivyoko katika Kata ya Mayo Halmashauri ya Bumbuli wenye gharama ya shilingi 531.8
Alisema mradi huo wa maji katika vijiji hivyo unatarajia kunufaisha wakazi zaidi ya  5,621 kutembea umbali mrefu kusaka maji hatua ambayo iliungwa mkono na Kiongozi wa Mbio za Mwenge na aliwataka wananchi kuilinda miundombinu ya mradi huo wa maji.
Sizinga aliendelea kusema kuwa fedha za Uviko 19
Shilingi milioni 250.7 ziliweza kunufaisha mradi wa maji uliopo Halmashauri ya Lushoto na kunufaisha wakazi wa vijiji 8 vya Kwesimu ,Kitopeni ,Jegestali,Lushoto Mjini Magereza ,Hazina,Mabwawani na Chake Chake.
Alisema mradi huo unaweza kunufaisha wakazi 5,427 na mradi huo unatarajia kuzalisha Lita 432,000 kwa siku na kutakuwa na ongezeko la upatikanaji wa maji kutoka Lita 2,288,838 kwa siku hadi Lita 2,720,838 kwa siku katika mji mzima wa Lushoto.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Sahili Geraruma aliipongeza RUWASSA kwa kutumia vema pesa za UVIKO 19 katika kunufaisha wakazi wa Wilaya ya Lushoto na kusema kuwa Mamlaka zingine zinapaswa kuiga kutoka kwa Mamlaka hiyo Mkoani Tanga.
Alisema changamoto katika miradi hazikosekani lakini kwa RUWASA ni tofauti Sana hivyo aliwataka viongozi wa Mamlaka za maji kujipanga kuhakikisha kilio Cha wananchi juu ya ukosekanaji wa Maji kinapungua ama kumalizwa kabisa màana Rais Samia suluhu Hassan anatoa fedha hivyo fedha zitumike ipaswa kwa maslahi ya Nchi.
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro Amepongezwa na kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa kwa usimamizi wa miradi mikubwa ambayo serikali imeweka pesa kwani zimekutwa na sifa ya kuzinduliwa bila kuwepo na ubadhirifu wowote wa pesa za serikali .
Mwisho