Site icon A24TV News

MWENGE WAZINDUA MIRADI YA BILIONI 5.2 LUSHOTO

Na Geofrey Stephen,Lushoto

Miradi 18 ya Elimu,Afya,Barabara na Maji yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 5.2 imezinduliwa na mbio za mwenge katika Wilaya Lushoto yenye Halmashauri mbili za Bumbuli na Lushoto Mkoani Tanga.

Akisoma taarifa mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Sahili Geraruma ,Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Kalist Lazaro alisema katika Halmashauri ya Lushoto mwenge umekimbizwa Kwa km 359 na kuzindua miradi 11 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.4.

Lazaro alisema katika Halmashauri ya Bumbuli Mwenge ulizindua Miradi ya Maendeleo 7 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.8.

Mkuu huyo alisema Miradi yote imezingatia thamani ya pesa,Ubora wa Kiwango cha majengo na kufuata Kanuni na taratibu za manunuzi.

Akizungumza mara bàada ya kuzindua miradi na kuweka jiwe la Msingi katika Miradi kadhaa Geraruma aliwataka watendaji wa Halmashauri kote Nchini kuhakikisha Miradi yote inazingatia thamani ya pesa na kuwa katika Ubora na kuwataka watendaji kuacha ubabaishaji na kufanya kazi Kwa mazoea hilo halitakubalika.

 

Geraruma alisema Rais Samia Suluhu Hassani anatoa pesa Kwa ajili ya Miradi mbalimbali Nchini hivyo Watendaji wa Halmashauri isiwe sehemu ya wao kufanya mambo kiholela na kutumia pesa katika Miradi ikiwa chini ya Kiwango hilo hatalivumilia.

Alisema na inasikitisha kuona Mtendaji idara ya Injinia aliyeisomea kazi yake na kupata elimu ya juu anafanya mambo kinyume kabisa na utaratibu na kusema kuwa watendaji wa namna hiyo wanapaswa kuachia ngazi kwa kuwa wanamkatisha tamaa Rais na hilo halitavumiliwa.

Mwisho