Na Geofrey Stephen Arusha
Katika jitiada za kulifanya taifa liweze kwendana na kasi ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu Taasisi ya Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha ( Arusha Technical College ) wameandaa na kutoa mafunzo ya siku nne kwa wanafunzi wa kidato cha tano na Sita katika Jiji la Arusha kutoka katika shule Saba zilizopo mkoani hapa
Hayo yamebainishwa na kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi Dkt Erasto Mlyuka wakati akifungua mafunzo maalumu ya siku nne ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu Kwa wanafunzi wa shule za sekondari ambapo alisema kuwa taifa la Tanzania ili likue katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia kuna ulazima wa kuwaandaa wataalamu toka mashulenni.
Alisema kuwa mradi huo ulianzia kwenye vituo vya kitaaluma ili kukuza mawazo na kuyapeleka katika ubunifu na pia kuyabadilisha na kuwa bidhaa na kisha kuyapeleka sokoni na kutumika kwenye jamii.
“Tulianza programu hii na shule 5 kwa mwaka 2017 na tulikuwa na wanafunzi 40 Mpaka sasa tunao wanafunzi 85 na shule 17 pia tulianzia jijini Dar es salaam lakini sasa tupo Arusha ambapo awali Kwa Arusha Tulianza na shule tano na Sasa tumeongeza mbili kwahiyo Kwa hapa Arusha tu tunashule Saba zilizopo katika programu hii “. Alisema Dk Mlyuka.
Dkt Mlyuka alisema kwamba, ili kufanikisha ubunifu na kupata matokeo chanya kunatakiwa kuwe na ushirikishwaji wa wataalamu mbali mbali ambapo aliwataka wanafunzi hao kuwa wepesi katika kuomba ushirikiano kwa walimu wao pamoja na wataalamu walionao
kwa upande wake Meneja wa Mradi huo Josephine Sepeku, alisema kupitia mradi huo anaamini mafunzo hayo wataishi nayo kwa muda mrefu na yatatoa matokeo chanya katika masomo yao na yatapelekea kuwa wabunifu wazuri na wataalamu wazuri katika nchi.
Alisema madhumuni ya mradi huu hasa ni kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na mradi huu wa sayansi ubunifu na biashara utawasaidia sana wanafunzi hao kuweza kukuza mawazo yao ya kisayansi kuyapeleka zaidi katika biashara ambapo alibainisha kuwa
tunapo sema Tanzania ya viwanda ili kuwe na viwanda lazima tuwe na wataalamu wa kutoka ndani ya nchi na ndiyo maana wameanza kwa kutoa mafunzo ya nadharia ili kuzidi kuwajengea uwezo toka wakiwa mashukeni na Baada ya hapo ifikapo mwezi December shule zote shiriki ziata shindwanishwa na washindi watapata mafunzo zaidi ya wiki sita ili kuzidi kuwaboresha zaidi katika ubunifu zao
Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha Arusha Technical Dkt. Yusuph Mhando, alisema kwamba wamekuwa wakitoa mafunzo mbali mbali katika chuo cha ATC na wanafunzi wamekuwa ni bora zaidi na anategemea mafunzo hayo yatawajenga vyema katika elimu yao.
“Chuo chetu kimekuwa daraja bora kwa wanafunzi wote wanao pita hapa kwaajili ya kujifunza mambo mbali mbali hasa katika ufundi, ubunifu wa kisayansi kwakuwa nyie mmeonyesha dhamira nzuri ya kuwa sehemu ya kuendelea kujifunza nina imani kubwa sana mtakuwa sehemu ya mafanikio ya kupata wataalamu mbali mbali katika nchi yetu hasa katika maswala ya uwekezaji wa viwanda”. Alisema Dkt Muhando