Wananchi wa kata ya Daraja Mbili jijini Arusha kwa pamoja wamekubaliana na kauli za Viongozi wao wa kata Akiwemo Mh Diwani wa kata Hiyo Prosper Msofe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo kubomoa Nyumba zao Wenyewe kupisha bara bara ya Lami
Wakizungumza na vyombo vya Habari wananchi hao wamesema wamekubaliana kwa kauli moja kubomoa nyumba zao pembe zoni mwa bara bara kupisha ujenzi wa bara ya kiwango cha lami inayo fadhiliwa na World Bank
Wananchi hao wamesema wamefuraishwa na jitiada za Mh Rais kuwaletea Maendeleo katika kata jambo ambalo linaleta maendeleo katika kazibya kata na wananchi kupata maendeleo ya araka
Wamesema wanampongeza sana Mh rais pamoja na Mbunge bila Kumsahau mpambanaji wao Diwanin Msofe ambaye katika ahadi zake za kuomba nafasi ya kuwatumia aliwaidi kuleta bara bara ya lami na ametimiza hilo
A24Tv imeshuhudia zoezi hilo wananchi wakibomoa nyumba zao wenyewe huku wakiamasisha wananchi wenzao kutimiza zoezi hilo mapema kwani kufikia tarehe 1 mwezi july 2022
Kwa upande wake Diwani Prosper Msofe Amesema anamshukuru sana Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitiada zake za kuakikisha wananchi wanapata bara bara kuanzia ngazi ya mtaa hadi kata.
Msofe amesema kinachofanyika kwa sasa ni jitiahada za kuakikisha kata yake inapata maendeleo kwa bara bara zake kua katika kiwango cha lami.
Mwisho .