Na Geofrey Stephen Arusha
WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), wamezitaka nchi wanachama kutimiza wajibu wao wa kuchangia bajeti ya jumuiya hiyo huku wakitilia mashaka kushuka kwa bajeti hiyo wakati idadi ya nchi wanachama ikiongezeka kufikia saba baada ya Jamhuri ya Kidemokradia ya Kongo kujiunga mwaka huu .
Waliyasema hayo mwishoni mwa wiki nje ya bunge muda mfupi mara baada ya mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa EAC, Betty Maina kusoma bajeti hiyo ya mwaka 2022/2023 ya dola za Marekani milioni 91.57.
Wabunge hao walisema kuwa bajeti hiyo imepungua ikilinganishwa na bajeti ya mwaka uliopita ya dola za Marekani milioni 91.78 wakati idadi ya nchi wanachama ikiongezeka kutoka nchi sita hadi saba.
“Ukijaribu kutazama miaka iliyopita unaweza kusema janga la UVOKO 19 limechangia kushuka kwa bajeti lakini kuna nchi wanachama wasiotoa michango yao, utaona japokuwa EAC imekuwa zaidi kwa kufikia wanachama saba sasa lakini bajeti inakuwa finyu,” alisema Ndangiza na kuongeza.
….Tunafurahia kukua lakini tunawaomba wanachama wa EAC wajue, kuwa mwanachama si kwa jina tu, lazima utoe mchango wako ili hatua mbalimbali na mipango ya EAC iweze kutekelezwa ikiwa ni masuala ya amani, usalama, uongozi bora, miundombinu na programu mbalimbali ziweze kutekelezwa,”.
Ndangiza alisema EAC inaweza kujitegemea huku akitolea mfano wa Umoja wa Afrika, (AU) ambao unaundwa na nchi 53 za bara hili imeweza kujitegemea kutoka na kuchangia kwa 0.2 ya bidhaa zao zote zinazotoka nje hivyo kwenye bajeti ya matumizi wanachangia asilimia 96 .
Kwa upande wake mbunge wa EALA kutoka Tanzania, Mhandisi, Habib Mnyaa, alisema kuwa kwenye iliyopitishwa nchi wanachama wanachangia asilimia 59 tu huku wahisani wakichangia asilimia 41 jambo alilodai kuwa si sahihi.
Alisema kuwa fedha hizo kutoka kwa wahisani si za uhakika sana kwani kuna wakati mwingine huwa wanatoa na wakagi mwingine hawagoi kabisa hivyi kukwamisha utaekelezaji wa mipango ya EAC.
“Inasikitisha mpaka sasa zaidi ya miaka 21.. tokea kuundwa kwa EAC mipango yetu inategemea fedha za wahisani zaidi,” alisema Mnyaa.
Hata hivyo alisema kuwa hiyo asilimia 59 ya bajeti huchangiwa na nchi nne tu za Tanzania Kenya Uganda na Rwanda huku nchi za Burundi na Sudan ya Kusini zikisusua kwenye uchangiaji.
Mnyaa alienda mbali zaidi na kudai kuwa licha ya mkataba wa kuanzishwa kwa EAC kuwa wazi juu ya nchi zinazosuasua kutoa michango yao lakini wakuu wa nchi za EAC hawajataka kuzichukulia hatua nchi hizo huku akisisitiza kuwa wataenda kuipitia bajeti hii ili waje na maoni zaidi .
Alishauri kuwa kufuatia vita inayoendelea barani Ulaya kati ya Urusi na Ukraine alisema kuwa ni vema nchi za EAC zikawa na mikakati hasa kuzingatia usalama wa chakula kama zilivyofanya nchi za India na Malasia kwenye baadhi ya bidhaa zao kama ngano na sukari ambayo hawasafirishi nje ya nchi zao zinatumiwa na wananchi wao tu
Naye, mbunge wa EALA kutoka Kenya, Fatma Ibrahim, alisema bajeti ya mwaka huu inaonekana haijaongezeka ingawa majukumu yameongezeka jambo alilodai kuwa Inawezekana ni kutokana na hali ya uchumi wa kidunia kutokana na vita (Ukraine na Urusi) hivyo nchi haziwezi kuongeza kuwango cha kuchangia.
“Wamejipanga kumaliza shida biashara baina ya nchi wanachama ambapo mfano biashara baina ya Tanzania na Kenya iko juu na wamezidi kuweka mikakati ili izidi kukua,” alisema Fatma na kuongeza.
…Fedha ya kuwekeza kwenye sayansi na teknolojia imeongezeka kidogo Tume ya Sayansi na Teknolojia imeongezwa ili kukuza ubunifu miongoni mwa wananchi wa nchi wanachama,”.
Hii ni bajeti ya mwisho kwa bunge hili la nne lililoanxa mwaka 2017 ambapo
linalomaliza muda wake desemba mwaka huu.