Site icon A24TV News

KIPANGA AZINDUA SHULE YA KIMATAIFA JUMUISHI YA MFANO YA SEKONDARI PATANDI ARUSHA.

Geofrey Stephen .Arusha

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga amesema kuwa serikali imeondoa vikwazo vya kimfumo na kimuundo kwaajili ya watu wenye mahitaji maalum nchini

Kipanga aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Shule ya Kimataifa Jumuishi ya Mfano ya Sekondari Patandi.

Alisema serikali imeondoa vikwazo hivyo ili kuwezesha utoaji wa elimu jumuishi kuanzia ngazi zote hadi vyuo vikuu ikiwemo kutambua mfumo wa elimu jumuishi kunawafunzi bado hawajapata elimu hiyo kwa shule maalum.

Waziri kipanga akizungumza na wananchi waliojitokeza katika afla ya uzinduzi huo wa shule ya kimataifa jumuishi 

Alisema serikali ya awamu ya sita iwezesha ujenzi na ukarabati wa ununuzi na usambazaji wa vifaa ikiwemo vifaa muhimu kama fimbo nyeupe,na vifaa vingine ikiwemo kuandaa kamusi maalum ya lugha za alama ikiwemo kuwalipia bima wanafunzi zaidi ya 120 wenye mahitaji maalum

Alisema pia miuongozo mbalimbali imewekwa ikiwemo kuhgaramia utoaji wa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi kidato cha sita na kuongeza kuwa shule hiyo umeleta chachu ya kutatua changamoto kwa wananza hao ili kuwasaidia wanachuo cha ualimu Patandi kufanya mafunzo kwa vitendo.

“Tukishirikiana kwa pamoja serikali na wadau kutainua ufaulu kwa wanafunzi hawa ikiwemo kujifunza kwa ufanisi”

Alisema shule hiyo iliyojengwa kwa sh,bilioni 3.835 imejumuisha maabara,nyumba za walimu,vyumba vya tehama,vifaa vya kufundishia vya kisasa pia shule hiyo jumuishi inajumla ya walimu 13 na wanafunzi wasioona wapo zaidi ya 71 kati ya wanafunzi 288.

Alitoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili waweze kuhesabiwa kwaajili ya kutatuliwa changamoto zao

Aliwashukuru wahisani mbalimbali waliosaidia shule hiyo kukamilika ikiwemo kutatua changamoto mbalimbali za kielimu ikiwemo uwepo wa karakana za kutosha ili kuwezesha watoto hao kujifunza zaidi kwa vitendo kwani watoto wenye ulemavu wanajifunza zaidi kwa vitendo hivyo mafunzo kwa vitendo ni muhimu kwa maendeleo yao.

Naye Dk,Magreth Matonya ambaye ni Mkurugenzi Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu,alisema shule hiyo ya Elimu Jumuishi ya Patandi ni ya Kimataifa na ni rafiki Kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum

Aisema shule hiyo imejengwa baada ya kutokea ukosefu wa madarasa ya usimamizi wa elimu jumuishi na shule hiyo ya Patandi imejengwa kama maabara kwaajili ya walimu wanaosoma Chuo cha Patandi kufanya mazoezi kwa vitendo kwaajili ya watoto wenye mahitaji maalum.

Alisema shule hiyo ilianza kujengwa Novemba,2017 huku thamani ya mradi ikiwa ni sh,bilioni 3.835 ikiwa na jumla ya madarasa 12 yenye vioo vinavyopelekea mwalimu kubaini changamoto za wanafunzi.

“Shule hii ni ya kimataifa na ni sekondari ya kwanza kujengwa yenye miundombinu ya kimataifa,tunamshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata haki ya kusoma”

Aliongeza kuwa shule hiyo pia inamabweni manne yenye vyumba vinne vinne huku kukiwa na vifaa maalum haswa kwa watu wenye ulemavu wanaohitaji vitu mwendo (wheel chair) na inajumla ya wanafunzi 288 miongoni mwao ni watoto viziwi,wasioona na wenye ulemavu mbalimbali

Na kusema kuwa kunawanafunzi wasioona wanaonekana kuwa na umri mkubwa kwasababu wanasoma miaka 10 wakiwa shule za msingi pia shuleni hapo wanafundishwa ujuzi mbalimbali unaowaandaa kujiajiri hapo badae.

Huku Mbunge wa Arumeru Mashariki,John Pallangyo alimpongeza Rais Samia kwa kujenga shule hiyo inayosaidia wanafunzi jumuishi kupata elimu ikiwemo jimbo hilo kupata fedha kwaajili ya maendeleo mbalimbali ikiwemo kutatua kero ya maji na kutoa rai kuwa Jimbo hilo kuongezewa shule nyingine ya sekondari badala ya Kisimiri Juu pekee ijengwe nyingine eneo la King’ori.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mhandisi,Richard Ruyango aliishukuru serikali kwa kujenga shule hiyo jumuishi ya mfano yenye watoto wenye mahitaji maalum kwani imekuwa ni chachu kwa watoto hao kusoma.

Alitoa rai kwa wazazi na walezi kutowaficha watoto wenye mahitaji maalum bali wawapeleke shule wakasome ili wawe viongozi bora badae

Wakati huo huo, Ofisa Elimu Sekondari Mkoa wa Arusha,Abel Mtupwa aliishukuru serikali kujenga shule hiyo ambayo wazazi wengi wanaitaka kwaaajili ya kusomesha watoto hao kutokana na uwepo wa miundombinu Bora.

Aliiomba serikali kuendelea kujenga shule nyingine kama hizo katika kanda mbalimbali ili kuwezesha watoto wenye uhitaji kujitokeza kusoma