Site icon A24TV News

MADEREVA 35 BARANI AFRIKA KUCHUANA VIKALI KATIKA MBIO ZA MAGARI ARUSHA

Na Geofrey Stephen Arusha

Mzunguko wa Nne 4) wa Mashindano ya Magari ya Afrika unaofahamika kama Africa Rally Champion Ship Mwaka 2022 unatarajiwa kuanzia July 22 hadi 24 mwaka huu katika eneo la Monduli Mkoani Arusha ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Mashindano hayo kufanyika Nje ya Mkoa wa Pwani.

Klabu ya Mbio za magari Arusha kwa kushirikiana na chama kinachosimamia Mashindano ya mbio za magari Tanzania (AAT) kwa pamoja watafanya Mashindano hayo yanayofahamika kwa jina la Tanzania Atlantic Rally ambayo yanajumuisha na ligi ya ndani ya mbio za Magari mzunguko wa Tatu

Mratibu alisema.Shindano hayo Satinder Birdi kando na kuwashukuru wadhamini ameelezea umuhimu wa Mashindano hayo ni pamoja na kuhamasisha maendeleo ya Mchezo wa Mbio za Magari

Aidha alisema kuwa jumla ya madereva 35 watashiriki katika mashindano hayo kati yao 13 wanatoka katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo saba kutoka Kenya Moja kutoka Zambia ,mmoja kutoka Rwanda ,wawili kutoka nchini Uganda na huku wengine wote waliobaki wakitokea nchini Tanzania.

“Kitu kinachofurahisha zaidi katika mashindano ya mwaka huu tunakivutio cha kipekee ambacho bila shaka mashabiki wengi watafurahia kwani mashindano haya yamebahatika kumpata mshiriki mmoja mwanamke ajulikanaye kwa jina la Maxin Wahome ,tunaamini atakuwa kivutio sana kwa mashabiki”alisema

Akizungumza kwa niaba ya wadhamini,mwakilishi wa Kampuni ya Atlantic Lubricants Sharan Aggarwal aliwataka wadhamini zaidi wajitokeze ili kukuza mchezo huo ambao unaonekana kuimarika kwa kasi,huku akibainisha kuwa mashindano hayo yataazia katika viunga vya hoteli ya Mount Meru Arusha na kuelekea wilayani Monduli

Kwa upande wake meneja wa hoteli hiyo Jonathan Cox ametoa wito kwa washiriki na Mashabiki kujitokeza kwa wingi kushiriki na kujionea mashindano hayo.

Naye Afisa Usalama wa Mashindano hayo Goodluck Mariki aliwataka washabiki pamoja na madereva kuchukuwa tahadhari zote za kiusalama pindi wanapo kuwa katika mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na maagizo yote wanayopewa na watu wa usalama

Aidha alitaja baadhi ya magari ambayo yatakuwepo katika mashindano haya kuwa ni Ford fiesta Rs, Mitsubishi Lancer Evo x,,Subaru Impreza, Skoda proto pamoja na Hyundai 120 R5 ambayo ndio gari pekee ambayo inaingia katika mashindano haya kwa mara ya kwanza.

Alibainisha kuwa mashindano ya ni ya mbio za magari ya Afrika ambayo nia yake ni kumtafuta dereva mmoja ambaye ataongoza kwa ushindi kwa nchi za Afrika na hii ni raundi ya nne tangu kuanza kufanyika ,hadi yalishafanyika katika nchi ya Kenya ,Zambia ,Ivory coast na raundi hii ya nne inafanyika nchini Tanzania mkoani Arusha

Katika Msimu huu Mashindano hayo yanategemewa kuwa na ushindani Mkubwa kutoka kwa madereva wa ARC pamoja na wale wa NRC kila upande madereva nguli kushinda Rally moja moja katika mizunguko yote.