Na Mwandishi wa A24Tv Munduli .
Fredrick Lowassa amesema Fedha zinazotumika katika ujenzi huo ni Fedha zilizotoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenda kwa Wabunge ambapo yeye ameelekeza Fedha hizo kutumika katika ujenzi wa barabara ndani ya wilayani hiyo.
Kwa Upande wake Eng Janeth Mkoreha Meneja Tarura -Monduli, amewahakikishia Wananchi wa eneo hilo kukamilika kwa Barabara hiyo kwa Wakati pamoja na Mitaro kufanyiwa kazi kwa wakati.
Ukaguzi huo wa barabara umeenda sambamba na ukaguzi wa soko kuu la Monduli Mjini Ambapo Awali akizungumza Mwenyekiti wa soko hilo Josephat Mbilinyi ameomba soko hilo kukarabatiwa , pamoja na malalamiko ya kutopewa mikopo kama wajasiriamali kutoka Halmashauri ndipo Mbunge Kumuagiza Mwenyekiti huyo siku ya Jumanne kufika ofisini kwake kwa ajili ya kuchukua fedha shilingi Millioni tatu na laki Nane (3.8) kwa ajili ya ukarabati wa paa la soko hilo.