Site icon A24TV News

MONGELA AZINDUA MWALIMU SPECIAl !NMB

Na Geofrey Stephen Arusha.

Wito umetolewa kwa Benki ya NMB hapa nchini kuhakisha inatoa elimu ipasayo kwa watumishi wa sekta ya Elimu  Walimu kuhusiana na Mikopo wanayoimba isije kuwashushuia morali ya  kufanya majukumu yao ya kufundisha wakiwa na hofu ya Mikopo wanayoikopa wakiofia riba kubwa.

Wito huo Umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mogella wakati akizindua huduma mpya ya Mikopo kwa walimu ‘ Mwalimu Spesho’ Katika Hotel ya Point Zone ya Jijini Arusha  ikiwa ni mikopo iliyoboreshwa kwa ajili ya Walimu pamoja na kuwa na Riba Ndogo Sambamba na kuwa na kipindi rafiki cha ulipaji wa mkopo huo.

Amesema kuwa Kutokana na Benki ya NMB kuzindua Huduma hiyo ambayo ni muhimu mkubwa sana kwa walimu ana matumaini kuwa italeta chachu ya maendeleo ya elimu hapa mkoani Arusha na hata nchi nzima kwa kuwa uwalimu ni sekta muhimu sana katika maendeleo ya nchi .

Aidha kwa upande wake Meneja wa huduma ya wateja binafsi wa Benki ya NMB Aikasia Muro amesema kuwa waliamua kuleta huduma hiyo mara baada ya kufanya uatafiti ulioshirikisha walimu wenyewe na kuona kuna umuhimu wa kuwarahishishia walimu huduma za kibenki kwa kuwapunguzia makali.

Amesema kuwa kuwa leo hii wamaezindua huduma hii ya MWALIMU SPESHO ambapo walimu watapata mikopo iliyorafiki kwa maana walimu ni wateja wa muda mrefu wa huduma ya benki ya NMB na hivyuo ni muhimu kwa Benki hiyo kutambua kuwawekea fursa hiyo ya walimu  kufurahia huduma zao.

Akitolea Mfano kwa Upande wa Mikopo hiyo ya Mwalimu Spesho kwenye upande wa kilimo wameshusha Riba ya mkopo wa kilimo hadi asilimia Tisa na zaidi wakiwa wameweka muda wa mpito wa kusubiri marejesho hadi pale mwalimu huyo aliyekopa atakapovuna mazoa yake.

Baadhi ya walimu walioudhuria uzinduzi wa huduma hiyo wamepongeza Benki ya NMB kwa kuwajali na kuwakutanisha kwa pamoja jambo ambalo limewafungua na kutambua huduma za kibenkI na wamesema kwamba watakua mabolozi kwa walimu wenzao katika kuakikisha kwamba wanatumia Benki kama sehemu ya maisha yao kwani hapo awali walikua wanajua kwamba wakipata imkopo watasumbuliwa na riba kubwa jambo ambalo wameona tofauti katika uzinduzi huo .

 

mwisho