Site icon A24TV News

RC Mongela Aionya Halmashauri ya Arusha DC Aitaka kuongeza Mapato

Na Mwandishi wa A24Tv.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameionya Halmashauri ya Arusha DC kuacha utegenezi wa fedha kutoka serikali kuu na kujikita kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo.

Mongela Ameyasema hayo kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa Kwa miezi mitatu serikali kuu isipoleta fedha Halmashauri hiyo inaweza kufungwa tafsiri halisi ya CAG asilimia 87 inatoka serikali kuu ambapo Halmashauri hiyo uwezo wake ni asilimia 13

Alisema kwamba Halmashauri ijadili jinsi ya kujenga uwezo wa mapato yake ya ndani kwa kuwa ni mzigo na haikutakiwa kuwepo Kutokana na utegenezi wake kwa serikali kuu.

“Hii ni Tafsiri ya Mkaguzi Mkuu wa serikali CAG uwezo wa halmashauri kuhimili kujiendesha ni asilimia 13 tu na utegemezi wake kwa serikali kuu ni asilimia 87 serikali ikiamua kutoleta fedha kwa miezi mitatu hamna Halmashauri kwa Tafsiri rahisi ni mzigo”

Aidha Mongela amesema kwamba Kwa kuwa ni wajibu wa kimsingi wa kikatiba kugatua madaraka ndio maana serikali kuu inawajibu wa kutafuta fedha za Kuendesha Halmashauri hiyo waheshimiwa madiwani uwezo wetu upo chini Halmashauri Ina uwezo wa kuongeza mapato maelekezo yapo kaeni chini kuongeza mapato

Alisema Ukitizama huku ndani ni mfumo Mkurugenzi ni kazi yako kuwa mbunifu vyanzo ni vile vile hakuna Ubunifu na matokeo yake hata fedha zinazoletwa mahitaji yanazidi hakuna Ubunifu uwezo ni mdogo na matokeo yake unapeleka kwenye sehemu nyingine

Amesema kwamba Mwenyekiti itisha kikao kujua miradi inayobuniw na kutelezwa ndani ya Halmashauri hii uone kama Kuna fedha za ndani zaidi ya fedha hizi za serikali kimsingi hatuna uwezo wa kimapato lakini tuna uwezo mkubwa wa kuanzisha mapato

“Mkurugenzi Huna vyanzo vipya vyanzo vilevile na vyanzo vilivyopo vimepitwa na hakuna Ubunifu hivyo hakuna uwezo wa mapato, hamna uwezo wa mapato uwezo ni mdogo vyanzo vipo vingi vyanzo ni viwili tu vya soko la karoti haiwezekani acheni urasimu”

“Kwenye mambo ya Msingi kupishana sioni tatizo Lengo liwe kuongeza mapato kubuni vyanzo vipya hivyo nisisitize suala la kujenga mapato ya Halmashauri lakini kwenye hoja hizi zipo za kizamani hakuna kitu kigumu kama umaskini ila nyie ni malofa”

Mwisho