Site icon A24TV News

RC MONGELA AWATAKA VIJANA KUA WAZALENDO KUWAENZI MASHUJAA

Na Geofrey Stephen , Arusha

Mavetenari waliopigana  Vita vya Kagera  (leo) wameadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kuweka silaha za jadi kwenye bustani ya Mnara wa Mashujaa Jijini Arusha.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana sambamba Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Irrange,Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella,viongozi wa dini pamoja na wananchi.

Akizungumza mara baada ya uwekaji wa silaha za jadi ikiwemo ngao,mkuki,shoka na sime,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mongella alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo ndani ya nchi kwakuhakikisha wanalinda amani na kudumisha mashikamano.

Ambapo Luteni Mstaafu,Allais Robert ambaye alicha nafasi yake ya uhasibu na kwenda kupigana vita vya Kagera mwaka 1978 hadi 1979,alisema wakati alipokuwa akienda vitani alikuwa na hamasa kubwa ya uzalendo wa nchi.

Alisema alipokuwa akienda kupigana vitani alikuwa na umri wa miaka 24 na alikuwa tayari kuendana na hali halisi ya mazingira waliyokutana nayo vitani.

“Wakati wa vita tulipata msaada kutokana kwenye vikosi mbalimbali vya majeshi yetu kutoka vyuo mbalimbali na tulijitoa kwa hali na mali kupigania nchi yetu na kumng’oa Nduli Idd Amin ”

Alitoa rai kwa vijana kutokimbilia tamaa za fedha na maisha mazuri badala yake wafanye kazi kwa bidii na kutanguliza uzalendo mbele.

Huku mmoja kati ya viongozi dini,Dk,Askofu ,Solomoni Masangwa wa Kanisa la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati (KKKT) alisisitiza amani na upendo ikiwemo kuwaombea viongozi wa serikali.

Ends…