Site icon A24TV News

Ruwasa yaokoa bilioni 57.4 miradi ya maji fedha kwenye miradi ya maji

Mwananchi wetu,Dodoma.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Nchini Vijijini (Ruwasa) imeokoa zaidi ya Sh57.4 bilioni ambayo ilikuwa itumike kugharamia miradi ya maji vijijini.

Fedha hizo zimeokolewa katika kipindi cha mwaka 2021/2022 katika miradi ya maji 86 ambayo ilikuwa itekelezwe kwa gharama ya Sh367.3 bilioni.

Mkurungezi Mkuu wa Ruwasa, Clement Kivegalo amesema hayo leo Jumanne Julai 19,2022 wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za taasisi na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Hapo awali ujenzi wa miradi ya maji ulikuwa ukifanyika kwa gharama kubwa ukilinganishwa na uhalisia. Kwa kutambua hilo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 ilifanya majadiliano ya kina ya mikataba na wakandarasi kwa miradi 86,”amesema.

Hata hivyo, Kivegalo amesema baada ya majadiliano na maelezo kuhusiana na miradi hiyo walitekeleza kwa Sh309.9 bilioni na hivyo kuokoa Sh57.4 bilioni ziliokolewa.

Kuhusu bei za maji, Mkurugenzi huyo amesema Agosti mwaka huu bei za ukomo wa maji zitaanza kutumika ili kuondoa malalamiko ya bei kubwa ya maji katika baadhi ya maeneo.

“Ruwasa itaendelea kufanya mapitio na maboresho ya bei za ukomo wa maji kila mwaka ili kuhakikisha bei za maji zinaendana na uhalisia wa gharama za uendeshaji kwa kipindi husika,”alisema.

Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Vijiji ilianzishwa na Serikali kutekeleza miradi ya maji vijijini na tangu imeanzishwa imefanikiaa kutekeleza miradi kadhaa ya Maji.
Mwisho