Site icon A24TV News

WATENDAJI WA WIZARA YA HABARI,MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI WAKUTANA ARUSHA KUWEKA MIPANGO YA KUTEKELEZA BAJETI

Moses Mashalla,

Watendaji mbalimbali wa wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari wanakutana jijini Arusha kuweka mipango ya kutekeleza bajeti ya wizara hiyo sanjari na kutathimini changamoto mbalimbali.

Hivi karibuni bunge la jamhuri lilipitisha bajeti ya wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari jumla ya kiasi cha sh,282.05 kama matumizi ya kawaida na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza katika kikao hicho naibu waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Mathew Kundo alisema kwamba wamekutana kwa lengo la kufanya tathmini na mpango wa kutekeleza bajeti hiyo ambayo ilipitishwa Hivi karibuni na bunge la jamhuri.

Naibu waziri huyo alisema kwamba mbali na kufanya tathmini hiyo pia wanaangalia maeneo mbalimbali ya kurekebisha katika bajeti hiyo.

“Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kituo kikuu cha habari na mawasiliano hivyo tumekutana kupanga mipango ya kutekeleza bajeti yetu “alisema Waziri Kundo

Hatahivyo,katibu mkuu wa wizara hiyo,Dk Jimmy Yonaz alisema kuwa mkutano uliowakutanisha ni muhimu kwa kuwa utaanisha mipango ,nia na kutoa dira njema kwa wizara hiyo.

 

Mkurugenzi wa magazeti ya serikali (TSN) Tuma Abdallah alisema kuwa mkutano huo unatoa fursa muhimu kwa watendaji wa wizara pamoja na wadau kukutana na kubadilishana mawazo namna ya kutekeleza shughuli mbalimbali ndani ya wizara hiyo.

Dk Abdallah alisisitiza kuwa mkutano huo pia ni muhimu kwa kuwa unatoa mwanga kwa watendaji kuzitazama changamoto mbalimbali na kusukuma maendeleo ya taasisi mbalimbali zilizoko ndani ya wizara hiyo na serikali kwa ujumla.

Mwisho.