YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa Udhamini
Geofrey Stephen
YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa Udhamini
KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani ya Tsh 12.3B kwa miaka mitatu (3), ambayo ni sawa na 4.1B kwa kila mwaka.
Hili ni ongezeko la Tsh bilioni 2 kwa mwaka kutoka kwenye mkataba awali wa bilioni moja kwa mwaka mmoja.
Sambamba na Fedha hizo ambazo Yanga itavuna, pia Bonus zitatolewa kama ilivyoainishwa kwenye mkataba ambapo Yanga ikifanikiwa kuwa Bingwa wa Ligi Kuu atapata Bonus ya 150M.
Yanga ikifanikiwa Nusu Fainali Azam Sports Federation Cup (ASFC) itapata Bonus ya 75M na endapo itakuwa Bingwa (ASFC) itapata 112M.
Mkataba wa awali kati ya Yanga SC na Sportpesa ulikuwa wa miaka mitano (5) wa Tsh 5.B sawa na Tsh 1 Bilioni kila mwaka katika kipindi chote cha mkataba yaani miaka mitano (5).
Rais wa Young Africans SC Eng. Hersi Said na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Ndg. Tarimba Abbas wakionyesha makubaliano ya mkataba mpya kati ya SportPesa na Young Africans