Site icon A24TV News

Halmashauri ya Arusha yamkabithi cheti cha shukrani  mfanyabiashara maarufu Monaban

Na Geofrey Stephen ,Arusha
Arusha.Halmashauri ya Arusha  kupitia baraza la madiwani wamemkabithi mfanyabiashara maarufu Dk Philemon Mollel (Monaban) cheti  cha  shukrani kwa kuchangia mifuko 60 ya saruji kwa ajili ukarabati wa  madarasa shule ya sekondari Oldadai katika halmashauri ya Arusha.
Akikabithi cheti hicho leo jijini Arusha katika baraza  hilo, Mkurugenzi wa  halmashauri ya Arusha   ,Suleman Msumi  amesema kuwa, wamefikia  hatua  ya kukabithi cheti  hicho kutokana na mchango mkubwa alionao katika shughuli mbalimbali za  maendeleo .
Amesema kuwa,walikuwa na zoezi la kitaifa  ambalo hufanyika  kila  mwaka la mwenge  wa uhuru kwa ajili ya kuweka  jiwe  la msingi na  kuzindua  baadhi ya miradi  ya halmashauri hiyo  iliyofanyika  julai  mwaka  huu.
“Tuliweza kushirikisha wadau  mbalimbali kuhusiana na swala letu  ambapo  Dk Philemon alifanikiwa kutupatia mifuko 60 ya saruji  kwa ajili ya kumalizia shule  ya sekondari Oldadai,na hivyo  kwa  kutambua  mchango  wake  tukaona ni  busara  kwa  halmashauri  kumkabithi  cheti  cha shukrani.”amesema Msumi.
Kwa upande wake,Mfanyabiashara huyo  Dk  Philemon Mollel ameshukuru sana baraza hilo kwa kutambua mchango wake  na kukumbuka  fadhila  kwa kumkabithi  cheti  cha shukrani jambo ambalo  linatoa  motisha wa  kuendelea kusaidia zaidi. 
Dk.Mollel amesema kuwa,kitendo kilichofanywa na halmashauri  hiyo  ni  jambo kubwa sana na linahitaji  kuigwa na taasisi zingine ili  watu  waendelee kuwa na motisha  wa kuisaidia  jamii  katika maswala  mbalimbali.
“Mimi niseme tu  nimefurahishwa sana kwa zoezi  hili  na kipekee naahidi kuendelea  kusaidia zaidi katika maswala  mbalimbali ya maendeleo  ili  jamii yetu  iweze kusonga mbele na kuondokana na changamoto mbalimbali. “amesema Mollel.
Mwisho.