Na Geofrey Stephen . Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi yana mchango mkubwa katika upatikanaji wa malighafi za nchi,na kuweza kupata masomo ya nje huku yakisaidia kuchangia ukuaji wa uchumi kwa maendeleo ya nchi.
Ameyasema hayo jijini Arusha ,kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati akifungua maonyesho ya kilimo na mifugo nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Themi Njiro yenye kauli mbiu ya”agenda 10/30 kilimo ni biashara ,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi”.
Alisema kuwa, maonyesho hayo yanatarajiwa kuchangia ukuaji wa mabadiliko kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali endapo elimu ya kutosha itatolewa na kuenea kwa elimu kwa jamii inayowazunguka juu ya killimo na ufugaji wa kisasa .
Aidha aliwataka watalaamu wa kilimo nchini kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na wafugaji ili walime na kufuga kisasa na kuepukana na kuondokana na zana za zamani na hatimaye kuweza kubadilisha maisha yao.
Naye Sheikh Shafi Muhammad MemonSheikh wa Mikoa wa Arusha, Kilimanjaro na Manyara Jumuiya ya Waislamu Wa Ahmadiyy alisema kuwa,maonyesho hayo yameshirikisha waonyeshaji 200 kutoka Taasisi mbalimbali licha ya taarifa kuchelewa juu ya uwepo wa maonyesho,lakini mwitikio bado ni mkubwa sana.
Aidha aliwaomba wananchi wa mikoa ya Kanda ya kaskazini kutembelea ili kujionea mambo muhimu kwa ajili ya wakulima na wafugaji ili kuboresha kilimo na ufugaji wao ikiwemo banda la jumuhiya hiyo ya waislamu kanda ya kazkazini kujipatia vitabu vya dini pamoja na ushauri wa maswala ya dini
Mwisho.