Site icon A24TV News

MFANYA BIASHARA WA MADINI ASHINDA TENA MWENYEKITI WA CCM KATA YA THEMI KWA KISHINDO

Na Geofrey Stephen .ARUSHA

Mfanyabiashara maarufu wa Madini jijini Arusha,Thomas Munisi amefanikiwa kutetea nafasi yake ya mwenyekiti wa ccm kata ya Them baada ya kushinda kwa kishindo akiwa safarini .

Katika nafasi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali ndani ya chama hicho, Munisi alishinda kwa asilimia 99 na kuwagaragaza wagombea wenzake wawili waliomfuatia kwa mbali.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,msimamizi wa uchaguzi,Kibuzo Senga alimtangaza Munisi kuwa mshindi wa nafasi hiyo na kuwashinda wagombea wengine ambao ni Feruz Ramadhani aliyepata kura 2 na Erick Mhalila aliyepata kura 2.

Senga alisema kuwa uchaguzi huo ni mwendelezo wa chaguzi za ndani za ccm ngazi ya kata zinaendelea hapa Arusha na aliwapongeza wajumbe wote kwa kushiriki uchaguzi huo na kufanikisha kuwapata viongozi salama bila kuwepo kwa manung’uniko.

Akiongea kwa njia ya simu Munisi aliwashukuru wajumbe wote kwa kumwamini na kumrejesha  kwa kishindo katika kiti hicho, kuendelea kukitumikia chama hicho.

Alisema siri ya ushindi huo ambao aliupata bila kuwepo kwenye uchaguzi ni uaminifu aliokuwa katika chama ikiwemo kukubali kujituma bila kujali unapata nini.

“Kimsingi niwashukuru sana wanachama wenzangu kwa kuniamini na kunichagua tena hii ni mara ya tatu nachaguliwa bila kuwepo na naimani kazi ninayoifanya inakubalika kwa wote”alisema.

Aliongeza  kwa kuwataka viongozi wengine wanaopata nafasi za uongozi ndani ya ccm kutotumia nafasi hiyo kujinufaisha bali wakisaidie chama katika kuwaletea maendeleo wananchi na kuacha kutumia madaraka hayo kama sehemu ya kujiongezea kipato.

Munisi alisema katika kipindi anagombea nafasi hiyo na kupata aliahidi mambo mbalimbali katikamkata hiyo ikiwemo kurejesha viwanda vilivyokuwa vimeporwa ,kukarabati ofisi iliyokuwa mbovu ,ahadi ambazo alisema amezitekeleza na sasa amejipanga kujenge ofisi mpya ya jengo la gorofa mbili katika kata hiyo.


Wagombea wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Deus Kitinde aliyetetea nafasi yake ya katibu ,Catherine  Nyabamba aliyetetea nafasi yake ya katibu uenezi.

Ends….