Site icon A24TV News

RC NJOMBE APIGA MARUFUKU WATOA MIKOPO UMIZA KUWARUBUNI WALIMU SHULENI

Na Emmanuel mkulu

Mkuu wa mkoa wa Njombe anthony_mtaka amesema ifike wakati walimu wasiendelee kutapeliwa na mikopo umiza ilihali walimu wamekuwa muhimu na wenye tija katika taifa.

Ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Programu ya benki ya NMB mkoani Njombe ya Walimu spesho ambayo amesema inapaswa iwe suluhisho la utapeli wanaofanyiwa walimu nchini.

vicky_bishubo Mkuu wa Idara ha biashara za serikali wa Benki amesema NMB Mwalimu spesho imelenga kuwasaidia walimu kupata mkopo wa kujiendeleza kielimu pamoja na kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 9 sambamba na mikopo ya biashara ndogondogo na bima.

Amesema benki hiyo inawatambua walimu kuwa ni watu muhimu katika jamii na wateja wao wakubwa hivyo imeona ni muhimu kuwaanzisha huduma ya Mwalimu spesho.

Baadhi ya walimu walioshiriki uzinduzi wa programu hiyo akiwemo Kilian Msemwa wamesema Programu hiyo itakwenda kuwafuta machozi kutokana na adha kubwa wanazokabiliana nazo kutoka kwa wakopeshaji fedha wa mitaani.