Site icon A24TV News

AFISA MADINI MKOA WA GEITA AWATAKA WADAU WA MADINI KUJITOKEZA KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Na Mwandishi wa A24Tv Geita .

_Aendelea kutoa huduma kwenye banda…_

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita Mhandisi Laurent Bujashi amewataka wadau wa madini katika mkoa wa Geita na maeneo ya jirani kutembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita.

Sambamba na kuwataka wadau wa madini kufika kwenye banda la Tume, akiwa katika banda hilo, ameendelea kutoa huduma mbalimbali kama vile vibali vya kusafirisha madini na kusajili wateja kwenye mfumo wa usimamizi wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (online mining cadastre transactional portal).

Matukio katika picha wadau wa madini wakipata maelezo kutoka banda la tume ta madini 

Akielezea Siku ya Madini iliyofanyika leo katika ukumbi mdogo wa Mwalimu Nyerere ikiwa ni sehemu ya maonesho amesema kuwa jukwaa limekutanisha wadau mbalimbali wa madini kwa lengo la kupeana taarifa mbalimbali na kubadilishana uzoefu katika Sekta ya Madini hususan Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini.