Na Geofrey Stephen .Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda leo Septemba Mosi amemtaka Mratibu wa zoezi la chanjo wilaya ya Arusha kuakikisha kwamba watumishi wote waliochaguliwa katika zoezi la kutoa chanjo ya polio na matone katika wilaya ya Arusha mjini wanalipwa stahiki zao zote mara baada ya zoezi hilo kukamilika.
Mtanda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa zoezi la chanjo ya matone kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano huku akisisitiza kuwa chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote kwa binadamu.
Pia amesisitiza kwamba zoezi hilo litadumu kwa siku nne hadi Septemba nne mwaka huu na kuongeza kuwa chanjo hiyo itawafikia hata wale walioko majumbani.
Akizungumza wakati wa kuzindua zoezi hilo katika kituo cha afya cha Levolosi Mtanda alisema kuwa kila mtumishi anaye shiriki zoezi hili la chanjo anapaswa kulipwa ujira wake mara baada ya kukamilisha zoezi la chanjo na matone kwani kumekuwepo na ubabaishaji wa watumishi kumaliza kazi yao na kuanza kusumbuliwa kulipwa ujira wao katika hili sintakubaliana nalo ,
“Mratibu na timu yako naomba watumishi hawa wakimaliza kazi hii wapewe ujira wao kulingana na makubaliano mlio weka sita penda kuona mtu ananifuata na kuanza kulalamila amekosa au amenyimwa ujiira wake kwa maaana hata maandiko yanasema kwamaba mlipe mtu ujira wake kabla jasho lake alijakauka ” Alisema Dc Mtanda huku watumishi wa zoezi ilo la Chanjo wakipiga makofi na vigelegele kuonyesha kufuraiya kauli hiyo ,
Katika hatua nyingine Mtanda amesema kumekuwepo na mvutano mwingi juu ya watalaam wa sekta ya afya kupitia jiji la Arusha juu ya kuboresha huduma za Afya katika upanuzi wa hospitali wamekuwa hawafanyi kazi zao na kufikia hatua hata fedha za maendeleo kurudishwa wizarani.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejitahidi kuboresha huduma za Afya na ikiwemo kituo hiki cha Afya cha levolosi Serikali ilitoa shilingi milioni 500. juu ya ujenzi wa kituo hiki sasa kumekuwa na mvutano juu ya ujenzi huo hadi fedha zilirudi kwa sababu ya watu wachache wanaotaka kukwamisha juhudi za Mhe Rais nikiwa kama mkuu wa wilaya hii sitikubali hata kidogo swala hilo litokee ndani ya wilaya yangu”. Alisema Mtanda.
“Nilikuja hapa zaidi ya miezi 3 nikawaomba tuwajulishe wizara ya mambo tuliyo kubaliana ili waturuhusu hizo fedha ziendelee na ujenzi sasa mimi niko hapa na sipo tayari kuwafurahisha wachache ni bora nyinyi wataalam mnione sifai kuliko kuwafurahisha nyie na wananchi waumie, nakuagiza mkurugenzi kwa kushirikiana na watalaam kuhakikisha ujenzi huo unaanza mara moja maana serikali imeshatoa pesa zaidi ya Bilioni 3.2 naomba fedha hizi ziweze kutumika na kuleta tija kwa wananchi wetu”. Alisisitiza Mtanda.
Zoezi la chanjo litaendelea hadi kufikia kilele chake tarehe nne mwezi huu wa september 2022
Mwisho