Site icon A24TV News

DC NJOMBE:KUACHA ARV NA KUKIMBILIA MITISHAMBA NI HATARI KUBWA

Na Emmanuel octavian

Watu wanaotelekeza matumizi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi ARV na kukimbilia kutumia dawa za asili(mitishamba)wameonywa vikali kwani kunaweza kuwasababishia madhara zaidi endapo dawa hizo hazitathibitishwa na mkemia mkuu.

Katika mkutano na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika kijiji Cha Lunguya mtwango wilayani Njombe mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema ni hatari kubwa kutelekeza dawa za ARV kisha kunywa dawa za mitishamba na kwamba jambo hilo linapaswa kupingwa kwa nguvu kubwa.

Mganga mkuu wa Halmshauri ya wilaya ya Njombe Dokta Suke Maghembe amekiri kuwapo kwa madhara juu ya kutumia dawa za asili ambazo hazijathibitishwa na kwamba watumiaji wa ARV wanapaswa kuendelea kuzitumia kwa malengo.

Katibu wa baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Gehazi Mhada anasema baadhi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wamekuwa wakikata tamaa ya kutumia dawa wakidai wamechoka jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao huku Jackson Kaduma ambay ni MVIU akisema kitendo cha kupima VVU mtu mmoja kwa majina tofauti na maeneo tofauti kunasababisha mkoa wa Njombe kuonekana kinara katika maambukizi ya vvu.

Roida Wandelage ni diwani viti maalum ambaye anasema vikundi vingi vya WAVIU vinapaswa kusaidiwa kwa mahitaji mbalimbali huku kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi.Tekla Sadala akiwaonya baadhi ya watumishi wa afya wenye tabia ya kuwakaripia waviu wanaokwenda kuchukua dawa.