Site icon A24TV News

MWENYEKITI MPYA WA TLP HUYU HAPA NI MKONGWE WA SIASA TLP ITAFIKA MBALI

Mrema alifariki Agosti 21, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa akipatiwa matibabu.

Uchaguzi huo umefanyika leo Ijumaa Septemba 9, 2022 katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, Hamad Mkadamu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho upande wa Zanzibar ameshinda kwa kura nne dhidi ya  mpinzani wake Dominata Rwechungura (Bara) aliyepata kura mbili kati ya kura sita zilizopigwa na wajumbe sita.

Akizungumza leo, Ijumaa Septemba 9, 2022 Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo baada ya kutangaza matokeo hayo amempongeza Hamad, amesema atakuwa anafanya kazi za mwenyekiti wa chama hicho hadi utakapoitwa mkutano mkuu wa kuchagua Mwenyekiti wa Taifa.

” Uchaguzi wetu ulikuwa na wagombea wawili ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Upande wa Zanzibar na Bara, Hamad ameshinda kwa kupata kura nyingi zaidi tutakuwa tunamuunga mkono kuhakikisha Chama kinaendelea kupiga hatua,” amesema Richard

Baada ya ushindi huo Hamad amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kwamba anajiona anajukumu kubwa la kuenzi mazuri yote yaliyoachwa na Hayati Mrema.

“Chama lazima kipige hatua, pamoja na shukurani zangu kwa wajumbe wenzangu kwa kuniamini bado nina kazi ya kuenzi mazuri yote ya mtangulizi wangu kwa kipindi chote na kuongeza mengine mapya kikubwa naomba ushirikiano,” amesema

Katika hatua nyingine Lyimo amesema Wajumbe hao wamemteua mtoto wa Mrema, Michael Mrema kuwa Mjumbe wa Sekretarieti kuu ya Chama hicho ikiwa ni kuthamini mchango alioutoa kiongozi wao huyo.

Mwisho .