Site icon A24TV News

NAIBU WAZIRI FEDHA AWATAKA MAAFISA MASUULI KUSHIRIKIANA NA KADA YA WAKAGUZI WA NDANI KUKUZA UTAWALA BORA

Na Geofrey Stephen

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande amewataka Makatibu wakuu ndani ya Taasisi za serikali kuhakikisha wanawashirikisha kwa hatua zote wakaguzi wa ndani lengo liwe kuongeza
uwajibikaji uwazi na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma na ripoti ya CAG.

Ameyasema hayo Leo  jijini Arusha wakati akifungua semina ya siku tatu ya bodi ya wakaguzi wa ndani inayofanyika jijini Arusha,ambapo uwazi na
uwajibikaji katika kutoa huduma sanjari na kuongeza vifaa kuwashirikisha itasaidia kuongeza uwazi kwenye uwajibikaji.

Alisema kwamba tunapokwenda IIA ni jambo muhimu sana katika nchi yetu ikiwa ni Pamoja kwa viongozi wa serikali kuwasogeza karibu wakaguzi wa ndani kwa lengo la kusaidia kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma sanjari na utawala bora.

Amebainisha kwamba KOO hawezi kumkama NDAMA maziwa vilevile CAG anatakiwa kuangalia sana taarifa za wakaguzi wa ndani kuweza kwenda sambamba katika ripoti ili kujenga mahusiano yenye lengo la utawala bora kwani yeye ni baba nan jia yake inaanzia humo.


“Utakuta baadhi ya mambo wakaguzi wa ndani hawashirikishwi bali inapokuja taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali mzigo wote anabeba
mkaguzi huyu wa ndani hivyo nitoe rai kwa maafisa masuuli wa serikali.

kote nchini wakiwemo Makatibu wakuu wa wizara kujenga mashirikiano ya karibu ili kuwa na mifumo mizuri ya utawala bora”.

Kwa Upande wake Rais wa Taasisi ya wakaguzi wa nbdani nchini Zelia Njeza amesema kwamba  kada ya ukaguzi wa ndani inasimamia mifumo ya utawala bora kama taratibu zilivyowekwa na serikali hivyo ushirikiano
unahitajika ili kuondoa changamoto za mdhibiti wa serikali na kuweka uwazi wa taarifa zinazotolewa.

Alisema kwamba mkutano wao huo ni wakimataifa na umeshirikisha mataifa mengine kujenga uweze na kutapa uzoefu jinsi mataifa mengine yalivyofanikiwa na utakuwa kwa siku mbili na baadae mkutano wao wa
kawaida utakaoanza siku ya Jumatano mkoani Arusha.

Alisema Serikali imeahidi itatoa ushirikiano ili kufanikisha mkutano wa kimataifa huku akiwataka maafisa masuuli kuendelea kushirikiana na
kada ya wakaguzi wa ndani ili kuweka uwazi na Utawala bora kwani wao ni jicho la nchi na taasisi na mdau wa wananchi.

Katibu Mkuu Wizara ya Aridhi Allan Kijazi Akizungumza na Vyombo vya Habari kuhusu Mkutano huo wa wakaguzi wa ndani ambapo amesema wanategemea sana baada ya mkutano huo kuona wakaguzi wa ndani wanaendelea kushirikiana na serikali kukuza uchumi wa nchi  kwani mkutano umelenga kua na majadiliano mengi ya kukuza uchumi wa nchi kufika pazuri

Mwisho .