Site icon A24TV News

POLISI NJOMBE WAKIRI KUNA SHIDA YA MIGOGORO

Na Emmanuel octavian

Wakati kituo cha sheria na haki za binadamu kikiweka kambi kutoa msaada wa kisheria mkoani Njombe katika maadhimisho ya miaka 27 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995 Jeshi la polisi limekiri kuwapo kwa migogoro mingi na mauaji yanayohitaji msaada wa kisheria toka LHRC.

Katika ufunguzi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe kupitia kituo hicho kwa muda wa siku 10 kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Butusyo Mwambelo anasema msaada wa kisheria unahitajika sana kutokana na matatizo lukuki yaliyopo katika jamii.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC,Wakili Fulgence Massawe ambaye ni mkurugenzi wa uchechemuzi na maboresho wa kituo hicho anasema tayari wamewafikia maelfu ya wananchi wenye matatizo mbalimbali na kuwapa msaada wa kisheria huku wakiadhimisha miaka 27 mkoani Njombe kutokana na utafiti kubaini kuwapo kwa changamoto nyingi katika mikoa ya kusini mwa Tanzania

Akifungua maadhimisho hayo ya huduma za msaada wa kisheria kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe,Katibu tawala mkoa Bi.Judica Omary amesema kwa kufanyika maadhimisho hayo mkoani hapa kutawapa fursa wananchi kupata huduma hiyo pasina gharama yoyote kwa maslahi mapana ya familia na taifa kwa ujumla

 

Mwisho