Site icon A24TV News

Serikali imeshauriwa kuwekeza nguvu kwa vijana hususani wajasiriamali wadogo wanaokuwa ili kuongeza Kasi ya viwanda nchini

Na Pamela Mollel,Arusha

Serikali imeshauriwa kuwekeza nguvu kwa vijana hususani wajasiriamali wadogo wanaokuwa ili kuongeza Kasi ya viwanda nchini

Kwa Sasa Kuna uwekezaji pamoja na mafunzo mbalimbali ambayo yanatolewa na SIDO ingawaje uhitaji bado ni kubwa sana.

 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Bilsarm Investment Ali Babu wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuhutimisha mafunzo ya mradi wa uanagenzi ambao ulikuwa unasimamiwa na SIDO

Alisema kuwa kwa Sasa uwekezaji ambao unafanywa umeweza kuzaa matunda makubwa na matunda hayo yanatakiwa yaweze kuifukia jamii hususani vijijini

Alisema kuwa endapo kama vijana wataweza kuwezeshwa kuanzia kwenye ngazi ya mafunzo wataweza kumiliki viwanda hivyo kuchochea ajira mpya kuzaliwa

“Fursa zipo nyingi sana lakini wakat mwingine namna ya kuzifuata fursa hizo inakuwa ngumu hivyo kama uwekezaji utakuwa kwa kiwango kikubwa utaweza kufanya fursa nyingi”aliongeza

Katika hatua nyingine aliwataka nao vijana ambao wamefanikiwa kupatiwa mafunzo pamoja na fursa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanazitumia fursa hizo ipasavyo sanjari na kubuni ajira mpya kila mara.

Akiongelea uwekezaji ambao ameufanya katika kiwanda Cha Bilsarm,alisema kuwa wao kama wadau wa kilimo wanajishugulisha na masuala mbalimbali ya kilimo

Alisema kuwa uwekezaji wake umeweza kuzaa ajira nyingi kwa kuwa wanachakata nafaka mbalimbali

“Sisi tunasambaza unga wa Dona,sembe,alizeti kwa kiwango kikubwa na kweli tunashukuru sana kwa kuwa mamlaka husika zimeweza kutuamini na Mimi niseme hii ni fursa kwa kuwa bidhaa zetu hizi tunaweza kuzisambaza hadi nje ya nchi”alisema

Alihitimisha kwa kuwataka watanzania kujijengea utamaduni wa kupenda bidhaa za ndani ambapo kama wataunga mkono jitiada hizo basi wamiliki wa viwanda wataongezeka