Na Mwandishi wa A24Tv Dodoma
Dkt. Kijaji ameyasema hayo Sepetemba 26, 2022 jijini Dodoma alipokutana na wadau wa sekta ya nguo na walio chini ya Chama cha Wazalishaji Nguo na Mavazi Tanzania (TEGAMAT) ili kujadili changamoto wanazokutana nazo.
Aidha, Waziri Kijaji amewashauri wadau hao kutokufunga viwanda, kwa kuwa ni sekta inayotoa ajira nyingi kwa vijana.
“Njoni tukae tuongee, tupange kwa.pamoja tuone cha kufanya, tunataka viwanda vifanye kazi katika Serikali ya Awamu ya Sita amnayo ni sikivu”. Amesema Dkt. Kijaji.
Aidha ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuona viwanda nguo vya Tanzania vinakua shindani na vinahudumia Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiongea mbele ya Waziri Kijaji, Katibu Mtendaji wa TEGAMAT Bw. Adam Zuku ameomba kuwe na ushindani wa haki na usawa kati ya waingizaji vitenge na wazalishaji ili waweze kushindana katika soko la nje
“Tunatamani kuhudumia soko la SADC,EAC, ACFTA” alisema Zuku.
Aidha, Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao wameiomba Serikali kuanzisha mitaala ya nguo kwa kuwa kwa sasa kuna uhaba wa wataalamu hao . Pia wameiomba tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali za Serikali kujumuishwa kwa pamoja ili kuwapunguzia usumbufu na gharama kubwa za uendeshaji.