Site icon A24TV News

MAIPAC kuwa na ushirikiano na Taasisi za CANADA,kusaidia jamii za pembezoni na Wanahabari.

Mwandishi wetu.Arusha.

Taasisi ya Wanahabari wa kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) inatarajiwa kuwa na mashirikiano na taasisi zisizo za kiserikali za nchini CANADA ili kuwajengea uwezo wanahabari na kusaidia jamii ya Pembezoni.

Mkurugenzi wa shirika la MAIPAC, Mussa Juma alitoa taarifa jana katika hafla ya kumuaga mshauri elekezi wa MAIPAC kutoka nchini Canada, Lori Legault ambaye alikuwa nchini kulijengea uwezo shirika la MAIPAC.

Mkurugenzi wa taasisi ya MAIPAC Mussa Juma akikabidhi cheti cha pongezi Lori Legault baada ya kusaidia mafunzo shirika hilo.

Juma amesema licha ya mshauri huyo kutoa mafunzo kwa MAIPAC jinsi ya kuandaa miradi na kutafuta wafadhili walifikia makubaliano ya kuwa na mahusiano na mashirika ya Canada ambayo yanajihusisha na kusaidia jamii za pembezoni na wanahabari.

Amesema mtaalam huyo ambaye ameletwa nchini maalum kusaidia MAIPAC na taasisi ya CESO kwa ushirikiano na ubalozi wa Canada ujio wake umekuwa na mafanikio makubwa.

Awali Legault alisema anashukuru kuja nchini Tanzania na kufanyakazi na MAIPAC kwani pia amejifunza utekelezwaji miradi ya MAIPAC .

Amesema amejionea kazi za mradi wa uhifadhi mazingira,Vyanzo vya maji na Misitu kwa maarifa asilia ambao unafadhiliwa na shirika la Maendeleo la umoja wa Mataifa(UNDP) na kusimamiwa na jumuiko la maliasili Tanzania(TNRF).

“nimefurahi kuwa Tanzania na MAIPAC watu wa Tanzania ni wakarimu sana na tutaendelea kushirikiana”alisema

Afisa Miradi wa MAIPAC Debora Makando alisema wamejifunza mengi kutoka kwa mfadhili huyo.

Makando alisema kutokana na mafunzo waliyopata wataboresha utendaji wa kazi wa MAIPAC.

Afisa Tawala wa MAIPAC Andrea Ngobole alisema wanahabari na jamii za pembezoni zitanufaika na mahusiano ya MAIPAC na Taasisi za Canada na CESO.

“tunataraji kuwa na miradi ya kubadilishana uzoefu kusaidia jamii za pembezo na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

mwisho