Site icon A24TV News

MILIONI, 500 ZAKAMILISHA KITUO CHA AFYA WANACHI WAMSHUKURU RAIS SAMIA

Na John Mhala,Bumbuli

Nyumba tano za Upanuzi wa Mradi wa Kituo cha Afya kata ya Mgwashi Jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga umegharimu zaidi ya shilingi milioni 247.6 hadi sasa

Nyumba hizo ni pamoja na jengo la Maabara,jengo la Mochwari,jengo la Upasuaji,jengo la Wazazi na nyumba ya Mtumishi ujenzi wa nyumba hizo umefikia hatua ya asilimia 80 kukamilika.

 

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mgwashi,Kelvin Shukia alisema mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ,Kalist Lazaro aliyetembelea mradi huo kuwa mradi ulikuwa ukamilike ndasni ya siku 90 ambapo ulikuwa ukamilike julai mosi mwaka huu.

Alisema lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika kutokana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wake na amemwomba Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anafuatilia changamoto hizo miradi hiyo inakamilika kwa faida ya wananchi.

Mganga huyo alisema wananchi walijitoa katika kusaidia ujenzi wa miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuchimba misingi na uandaaji wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo matano.

Alisema ili majengo hayo yaweze kukamilika zaidi ya shilingi milioni 252 zinahitajika na ameiomba serikali kukumbuka kupeleka fedha kwa ajili ya miradi hiyo ili wananchi waweze kupata huduma.

Mkuu wa Wilaya aliwahakikishia wananchi wa Mgwashi kuwa serikali haiataweza kuwaacha katika kumalizia majengo hayo na suala hilo atalivalia njuga na kuhakikisha fedha zinakwenda na kumalizia ujenzi wa majengo hayo.

Lazaro alisema ujenzi wa Kituo cha Afya Mgwashi ni mkombozi kwa wananchi 180,000 kwa sense ya mwaka 2012 waliopo katika kata hiyo na jimbo la Bumbuli kwa kuwa itawaondolea adha ya kuenda umbali mrefu kusaka huduma ya afya.

Alisema changamoto zote zilizoelezwa na Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya zitafanyiwa kazi na kila kitu kitakwenda sawa kwani serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan iko kwa ajili ya wananchi.

Mwisho