Site icon A24TV News

NABII DKT GEORDAVIE AMZAWADIA GARI LA KIFAHARI LA ZAIDI YA SH,MILIONI 100 MSANII MKALIWENU.

Na Geofrey Stephen ,Arusha

Katika hali isiyo ya kawaida mchekeshaji aliyejizolea umaarufu mitandaoni Jackson Sakwile maarufu kama “Mkaliwenu “ametunikiwa gari la kifahari aina ya BMW X5 na Nabii maarufu nchini Dk GeorDavie baada ya kukunwa na mashairi ya nyimbo aliyoitunga kwa ajili yake.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika eneo la Kisongo katika huduma ya Ngurumo ya Upako ambayo inaendeshwa na nabii huyo ambaye hivi karibuni amejizolea umaarufu kwa kutoa misaada na zawadi kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii.

Akihojiwa na waandishi wa habari mchekeshaji huyo amesema kwamba anamshukuru Nabii Dkt GeorDavie kwa kumzawadia gari hilo kwa kuwa hakuwahi kuwa na ndoto ya kumiliki gari lenye thamani kubwa kama hilo.

Mchekeshaji huyo mwenye mbwembwe amesema kwamba awali wakati akitunga na kisha kutoa nyimbo hiyo baadhi ya wasanii nchini ambao hakuwataja kwa majina walimdhihaki kwa kumwambia kuwa njaa itamuua lakini yeye alifanya hivyo kwa mapenzi kwa Nabii Dkt GeorDavie.

“Wasanii wenshangwe

nipondwa kwa kuniambia njaa itaniua lakini namshukuru Mungu amejibu maombi “amesema Mkaliwenu

Hatahivyo,amesisitiza kuwa anamkubali Nabii Dkt GeorDavie kwa kuwa mbali na mafundisho yake kuhusu kanuni za kumjua Mungu lakini pia anafundisha kanuni za kuondokana na umaskini.

Mchekeshaji huyo mbali na kupewa gari hilo la kifahari pia alizawadiwa kiasi cha sh,1 milioni za mafuta huku akisisitiza kwamba imani yake hatimaye imezaa matendo.

Awali katika mahubiri yake Dkt GeorDavie alisisitiza kuwa lengo la kumzawadia gari msanii huyo limekuja kutokana na imani na hivyo anastahili tuzo hiyo.

“Imani yake ni kubwa na anastahili reward (zawadi)na ninayainua maisha yako kwa kukuzawadia gari aina ya BMW X5”alisema nabii huyo huku umati wa waumini kanisani hapo ukilipuka kwa shangwe

Huu ni mwendelezo wa nabii mkuu Dkt GeorDavie kutoa zawadi mbalimbali kwa makundi mbalimbali kwenye jamii ambapo hivi karibuni ameonekana akitoa misaada ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo wadogo,bajaji,fedha za mitaji na magari kwa wasanii mbalimbali nchini kitendo ambacho kimemjengea umaarufu ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Mwisho