Site icon A24TV News

WAZEE 40, WAPATIWA MSAAADA WA KADI ZA AFYA ZILIZOBORESHWA

Na Julian Laizer Munduli .

Wazee wasiojiweza kutoka vijiji vya Mti Mmoja na Lashaine, Kata ya Sepeko na Lashaine wilayani Monduli mkoani Arusha wametatuliwa changamoto ya kimatibabu waliyokuwa wakiipitia kwa kipindi cha muda mrefu kwa kukabidhiwa kadi za bima ya Afya zitakazowasaidia kutibiwa bure.

Mbali na kadi hizo wazee hao wamekabidhiwa mashuka mazito kwa ajili ya kujifunika usiku na kuzuia baridi na hapa wanaeleza namna walivyotwaliwa mzigo wa matibabu.

Wakizungumza baadhi ya wazee , akiwemo mzee Lowasare Loderieki, Maria Saitoti na Leparakwo Melakiti , kwa pamoja wameshukuru shirika la DIVINE MERCY CARE AFRICA (DMCA) chini ya Mkurugenzi wake Lekoko Kipuyo Ngotieki kwa kuona umuhimu wa afya kwa wazee na kuwapa msaada wa kadi hizo.

“Zamani tulikuwa tukienda hospitali bila pesa hatupewi dawa, tunamshukuru mtoto wetu Lekoko kwa msaada huu wa kadi tunaamini hata sasa tunaenda kutibiwa bure. Tunamshukuru pia mtoto wetu Lekoko kwa kutufunika na blanket nzito hatutaumia tena na baridi “ wazee.

“Lakini pamoja na yote tunaomba serikali ituangalie na shida ya maji sisi wazee hatuwezi kufuata maji umbali mrefu, watuanglie kutatua changamoto hii tunateseka na ukame lakini pia njaa hata uji kwenye kibuyu hatupati tena. Hakuna unga, mahindi hakuna, tulilima hatujapata kitu je ukimwa ukipata hiyo dawa bure utatumiaje na uko na njaa? serikali yetu itusaidie msaada wa chakula “ wazee.

Kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo Mkurugenzi wa Shirika la DIVINE MERCY CARE AFRICA (DMCA), Lekoko Kipuyo Ngotieki ndiye anayeshikilia usukani wa kuwanusuru wazee hawa, amesema sababu zilizopelekea kulichagua kundi hili ni, ” wazee ni kundi lililosahaulika na wadau wengi hawajawekezeka katika eneo hili na pia kujali Wazee ni hazina, hivyo ni jukumu la kila mwanajamii kuwatunza”

“ Lengo letu ni kwa wazee na sasa tumewafikia wazee 40 kutoka kijiji cha Mti Mmoja kata ya Sepeko na Lashaine kata ya Lashaine lengo ni kuwafikia wengi na ikiwezekana Afrika nzima kulingana na jina la shirika lenyewe. Tunawasaidia pia wanawake hususani wajane, na hadi sasa tuna watoto 8 tunaowahudumia shuleni kwa kila kitu. Nawashukuru sana wadau wa wameendeleo akiwemo Lesley( Founder wa DMCA), Margo na Tina kutoka Australia walioonyesha nguvu zao hapa katika kutekeleza haya “.

Mwandishi wa habari hizi hakuishia tu hapo alikuwa na shauku kubwa kutaka kufahamu, je serikali wilayani Monduli inamikakati gani juu ya matibabu ya wazee?
Hendrich Emanuel Laizer ni Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, ambaye naye alielekeza shukrani kwa shirika DIVINE MERCY CARE AFRICA (DMCA), kwa kuwajali wazee kwani kadi hizo zimekuja wakati muafaka ambayo *Serikali nao wako kwenye uchakataji wa kuhakikisha kila mwananchi kuwa na kadi ya Bima ya Afya* na kuahidi kushirkiana na wadau wengine.