Site icon A24TV News

Waziri Ndumbaro WANANCHI WABORESHEWA MFUMO WA TEHAMA KATIKA UTOAJI HAKI NCHINI

Na Geofrey Stephen Arusha

Wizara ya Katiba na Sheria Imeeleza kwamba imejipanga katika mfumo wa
Tehama katika utoaji haki nchini utaosaidia kuboresha kurahisisha na
kuondoa changamoto za wananchi kufuata huduma umbali mrefu.

Aidha Serikali imeweka mazingira mazuri ya mfumo wa kidigiti kuweza
kupatikana katika Katiba na sheria sanjari na elimu mtandao ya sheria
ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa urahisi Popoto walipo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro
wakati akizindua mafunzo ya mifumo ya Tehama kwa sekta ya sheria kwa
wadau wa huduma za kisheria kwa siku mbili jijini Arusha.Alisema kwamba katika Bajeti ya mwaka huu waliweka vipaumbele 14
ikiwemo matumizi ya Tehama katika mifumo ya utoaji haki nchini na
kuanisha kuwa wameafanikiwa katika mhimili wa mahakama.
Kwa Mujibu wa Waziri Ndumbaro amesema kama wizara wanajukumu kubwa
katika utoaji wa elimi juu ya katiba na sheria kupitia Tehama pamoja
na kuweka mahakama ya mwanzo kila tarafa kurahisisha utoaji haki kwa
wananchi.Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha tehama wizara ya katiba na sheria
Gabriel Omari amesema lengo kubwa la mafunzo haya ni kuhakikisha wadau
wa sheria wanaweza Kutumia mfumo wa tehama kujisajili popote walipo
badala la kwenda wizarani sanjari na shughuli zote za wizara kufanyika
kwa njia ya Mtandao.
Alisema lengo la Mafunzo hayo ni kutoa uelewa mpana kwa washiriki hao
katika Tehama kwa kwa kuwa tokea kuanzishwa kwa mfumo huo kumekuwa na
changamoto ya uelewa hivyo kuchelewesha wananchi kupata huduma.Awali Msajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria Nchini Felista
Mushi amesema Mafunzo hayo yamewashirikisha watoa huduma za kisheria
kutoka mikoa 10 wasajili wasaidizi  pia kutoka mikoa kumi pamoja na
maafisa Magereza na Polisi waliopata mafunzo ya msaada wa kisheria.
Alisema kwamba washiriki hao wamechaguliwa kwa sababi wapo karibu na
wananchi sanjari na kuwasaidia wananchi wengi wa chini waliopo maeneo
mbalimbali nchin lengo ni wizara kuingia katika mfumo wa utoaji haki
hususani haki jinai kwa urahisi.