Site icon A24TV News

WIZARA YA HABARI TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO YAWAPIGA MSASA VIONGOZI WA VYUO MASWALA YA MTANDAO

Na Geofrey Stephen Arusha.

WIZARA ya Habari Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imewataka wananchi kutambua kuwa suala la uchunguzi wa simu zilizopotea katika
jeshi la Polisi nchini ni huduma ya Bure ambayo haina malipo yeyote.

Akizungumza na Uongozi na wanafunzi wa Vyuo vya Uhasibu IIA na Ufundi ATC jijini Arusha Mtaalamu wa Usalama wa mtandao na uchunguzi wa
makosa ya Kidigitali Yusuph Kileo amesema kwamba ipo haja kwa wananchi kujengewa uelewa wa matumizi salama ya makosa na uhalifu wa mtandao.

Kwa mujibu wa Mtaalamu huyo Uelewa huo utsaidia sana jamii kuelimishwa kuhusu sheria kanuni na miongozi inayosimamia usalama Mtandao hapa nchini wkati huu wa mageuzi ya kiuchumi kwa njia ya kidigiti.

Alisema kwamba wapo wengi ambao Nyilawila zao wamekuwa hawaziweki katika usalama na kupelekea wahalifu kutumia kurasa zao za mitandao ya
kijamii kiuhalifu hivyo busara kwao ni kuweza kujengewa uelewa utakaosaidia kuepuka na kuwa salama

“Hivi sasa serikali inaendelea kutoa elimu kwa wadau wake ndani ya serikali ambao utasaidia kuondoa uhalifu wa kuingia kwenye mifumo bila kuingiza nyilawila ya ofisa muhusika hivyo kama watu hawapati uelewa
na elimu kutakuwa na mianya ya uhalifu.

Kwa Uapnde wake   Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Musa Mhandisi Chacha amesema mafunzo hayo ya usalama kwa njia ya mtandao yatasaidia
kuongeza uelewa wa matumizi sahihi ya mitandao nchini na kuondokana na
uhalifu wa kimtandao.

Akatoa wito kwa Wizara kwanda kwa wananchi wakati huu uchumi ukielekea katika mitandao kutuma na kuagiza sanjari na malipo kwa njia hiyo
hivyo uelewa ukiwafikia wananchi utasaidia sana kuondoa changamoto wanazokumbana nazo.

Awali akiongea Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka wizara ya Habari teknolojia ya Habari na mawasiliano amesema kwamba tokea mwaka 2018 kazi ya kuangalia usalama mtandao nchini na maboresho yake umeendelea kufanyika na serikali.

Alisema kwamba ipo misingi mitano mikuu ya uboreshaji ambyo ni miundombinu wezeshi Teknolojia wezeshi Sheria wezeshi Utaalamu sanjari na mazingira ya udhibiti wao kwa sasa wapo katika kampeni ya kutoa
elimu na kuutambulisha mfumo huo wakati akijipanga kuwaendea wananchi.