Site icon A24TV News

AMANI GULUGWA ASHINDA TUZO YA WAKURUGENZI BORA

Na mwandishi wa A24Tv .

(Mr. Amani Golugwa ameshinda tuzo ya THE TOP 100 EXECUTIVE LIST 2022 TANZANIA AWARDS. Mr. Amani amekuwa mmoja wa washindi kwenye kundi la Wakurugenzi (CEO) wa Asasi za Kiraia (Mashirika yasiyo ya Kiserikali) na kutwaa tuzo ya MKURUGENZI BORA WA TAASISI KWA MWAKA (CEO OF THE YEAR 2022) katika mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs.

Mr. Amani Golugwa ni Mkurugenzi (CEO) wa shirika la Help to Self Help lililopo Jijini Arusha, ambalo linahusika na masuala ya Elimu (Ujuzi na Ufundi Stadi), Kuiwezesha Jamii (Economic Empowerment) na Afya (Community Health).

Tuzo hizo zilifanyika Jijini Dar es Salaam katka ukumbi wa Mlimani City tarehe 27 Novemba 2022 na kuhudhuriwa na Wakurugenzi zaidi ya 600 kutoka katika taasisi mbalimbali nchi nzima.