Site icon A24TV News

FRANK BATEZI NA NICO NGOWO MBARONI KWA KUBAKA, KULAWITI NA KUMUINGIZIA CHUPA MUUZA BAA

 

Na Mwandishi wetu, Mirerani

Wakazi wawili wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Frank Msuya Batezi na Nico Anthony Ngowo, wanashikiliwa na polisi kwa kumbaka msichana muuzaji wa baa na kisha kumuingizia chupa ya bia njia ya haja kubwa.

Batezi na Nico inadaiwa kuwa walishirikiana na wenzao wengine wawili ambao walikimbia, kumbaka na kumlawiti msichana huyo kisha kumuingizia chupa ya bia njia ya haja kubwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, George Mutabazi amethibitisha kukamatwa kwa watu wawili kwa kudaiwa kumbaka na kumlawiti msichana huyo.

Kamanda Mutabazi amesema wanatarajia kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao wawili wakati wowote ili wakajibu mashtaka hayo yanayowakabili kwani uchunguzi umekamilika.

Mmoja kati ya shuhuda wa tukio hilo, Hassan Juma amesema Batezi na Nico walikuwa wanakunywa pombe na msichana huyo eneo la Songambele kasha wakaenda Kazamoyo kulala.

Amesema walishirikiana watu wanne kumfanyia kitendo hicho cha kikatili kwa kumbaka, kumlawiti kisha kumuingizia chupa ya bia kwenye sehemu ya haja kubwa.

“Ni kitendo cha kinyama mno walichokifanya Batezi na huyu Nico ambaye ni raia wa Kenya kwani dada wa watu aliharisha na damu kuvuja kwenye njia ya haja kubwa,” amesema.

Mganga wa mfawidhi wa kituo cha afya Mirerani Dk Deogratius Mazengo amethibitisha kutibiwa hapo kwa msichana huyo ambaye alifika na fomu namba tatu ya polisi.

MWISHO