Site icon A24TV News

Maganya aitaka jumuiya ya wazazi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia.

Na Geofrey Stephen .Arusha
Arusha.Mwenyekiti wa wazazi Taifa (MCC) Fadhili Maganya ameitaka jumuiya ya wazazi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika maswala mbalimbali ya maendeleo anayoendelea kuyafanya .
Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akikaribishwa rasmi na jumuiya ya wazazi mkoani Arusha

Maganya amesema kuwa, Rais Samia amekuwa akifanya mambo mengi sana ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuyaunga mkono na kuhakikisha kazi inasonga mbele.

Amefafanua kuwa,wataendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa namna yoyote ile na yupo tayari kumtetea Rais na kamwe hatakubali kuona jina la mama linachezewa na mtu yoyote.

Aidha amesema kuwa, wanachotakiwa kutambua wao ni kuwa,kama kura zimetosha au hazijatosha warejee kujenga chama cha mapinduzi ,huku akiwataka kutoa ushirikiano wa kutosha kukisapoti chama .

Kwa upande wake Katibu wa ccm mkoa wa Arusha,Musa Matoroka amesema kuwa,wao kama jumuiya ya wazazi wanatakiwa kutafuta kura za ccm katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 pamoja na uchaguzi wa dola ifikapo 2025.

Naye Mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Arusha, Hezron Mbise amesema kuwa,jumuiya hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa nyuki ambayo imeleta manufaa makubwa sana .

Mwisho.