Na Emmanuel mkulu
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Adelina Ng’olo mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Nyombo wilayani Njombe kwa tuhuma za kuwachoma moto watoto wake wawili katika sehemu mbalimbali za miili yao kwa kile alichodai wamemdharirisha kwa kuomba chakula kwa majirani.
Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa Amewataja watoto hao waliochomwa moto kuwa ni Eliud Chatanda[7] na Elina Chatanda mwenye umri wa miaka[4] ambao walikwenda kwa majirani kutafuta chochote ili mradi siku iende lakini majirani wakaanza kumsema mama huyo kuwa anashindwa kuwalea watoto wao mpaka wanakuwa ombaomba
Aidha kamanda Issa anatoa wito kwa wananchi wa Njombe katika malezi ya watoto na kwamba ukatili huo hapaswi kufanyiwa binadamu yeyote hivyo ni muhimu kuachana na vitendo hivyo.
Edward Mlowe na Makwayi Barani ni wakazi wa Njombe ambao wanasema ukatili unaofanyika mkoani Njombe unapaswa kupingwa na kila mtu kwani hakuna sababu ya kuchukua hatua ngumu za kuwachoma watoto na kuwaharibia maisha yao badala ya kuwapa adhabu ndogondogo.
Mkoa wa Njombe umekuwa ukikumbwa na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mara kwa mara jambo linalosababisha athari za kimwili na kisaikolojia kwa watoto hao huku jamii ikitakiwa kuchukua hatua stahiki katika kupinga vitendo hivyo.