Site icon A24TV News

MONGELA AVUTIWA NA JENGO LA HOSPITAL CHUO CHA ATC LA BILION 1.384

Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella amekitaka chuo cha ufundi Arusha ATC,kuhakikisha huduma zitakazotolewa katika  mradi wa hospitali unaojengwa chuoni hapo,unaimarisha sekta ya afya  nchini  na kukidhi mahitaji ya afya kwa wanafunzi  , jamii na  watalii.
Akiongea mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa jengo la hospitali ya kufundishia na Tiba ( Polyclinic )katika chuo hicho ,alisema Kliniki hiyo ikikamilika isaidie kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wanafunzi kujifunzia na tiba kwa wananchi.
Alisema kuwa ubora wa huduma zitakazotolewa katika hospitali hiyo uwe wa kiwango cha juu na uendane na hadhi ya majengo na kukidhi huduma za afya kwa watalii .
“Niwapongeze sana kwa matumizi sahihi ya fedha za mradi nipo tayari hata kumleta rais Samia Suluhu kufungua jengo hili ninachowaomba mjitanzaze na sisi kama mkoa tutaendelea kuwatangaza”
Katika hatua ngingine Mongela alikipongeza chuo hicho kwa kutekeleza mradi huo kwa ubora na gharama nafuu ya sh,bilioni 1.384  na kuahidi miradi mingine ya serikali mkoani hapo kukipatia chuo hicho   kwani kimeonesha uzalendo na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.
Awali mkuu wa chuo hicho,Mussa Chacha alisema hospitali hiyo imetekelezwa na chuo hicho kupitia mapato yake ya ndani ,ambapo kiasi cha sh,bilioni 1,384,301,300 kilitengwa.
Alisema  hospitali  hiyo itatatua upungufu wa miundombinu ya kufundishia mafunzo  kwa vitendo ,tafiti nanhudumanbora za matibabu kwa wananchi wa jiji la Arusha.
Alisema kwa sasa hospitali hiyo imefikia asilimia 92,na kiasi cha sh,bilioni 1.064 kimetumika hadi sasa na ujenzi huo unatarjiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba, mwaka huu 2022 .
Alisema hospital  hiyo inakadiliwa  kutoa huduma kati ya  watu 100 hadi 300 kwa siku ikihudumia wanafunzi,wafanyakazi na wananchi  katika huduma za uchunguzi wa afya ,huduma ya mama na mtoto , huduma  ya macho,mfumo wa pua ,koo ,masikio ,meno magonjwa ya ndani ,huduma za upasuaji ,utoaji dawa na vifaa tiba.
Ends..