Site icon A24TV News

Mzuka Nusu Fainali Chemchem CUP 2022 kuanza leo kuwania mamilion Babati.

Mwandishi wetu, Babati

Mzuka wa Nusu Fainali ya michuano ya Chemchem CUP 2022, inatarajia kuanza leo, ambapo timu ya Mshikemshike FC ya vilima vitatu itachuana na Timu ya Macklion kutoka kijiji cha Mwada wilaya ya Babati mkoa Manyara

Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 16 kutoka katika vijiji 10 ambavyo vinaunda jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge zaidi ya sh 25 milioni zinatarajiwa kutumika, ambapo awali timu zote zilipewa seti ya jezi na mipira.

Nusu fainali ya pili ya michuano hiyo, timu ya Mdori FC ya kijiji cha Mdori itachuana na timu ya Mofuri FC ambayo pia inatoka katika kijiji cha Mdori.

Michuano hiyo, ambayo inadhaminiwa na Taasisi ya chemchem Association ambayo ni kampuni tanzu ya Chemchem ambayo imewekeza katika eneo hilo la Burunge WMA katika utalii wa picha na hoteli, imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu mwaka 2019 lengo za kuzuia ujangili katika eneo hilo na kutunza mazingira.

Mwenyekiti wa michuano hiyo, Erasto Belela amesema maandalizi yote muhimu ya michezo ya nusu fainali yamekamilika.

Amesema kabla ya timu hiyo kutinga nusu fainali, timu nyingine zilizofanikiwa kuingia robo fainali ni pamoja na Chui Fc, Manyara FC, Minjingu FC na Olasiti FC ambazo zote zinatoka katika vijiji vilivyounda Burunge WMA.

Belela amesema licha ya soka pia kutakuwa na michuano ya mpira wa pete ambapo bingwa atazawadia zaidi mbali mbali zinazofikia sh 500,000.

Katika michuano mwaka huu ni kupiga vita ujangili dhidi ya Twiga ambao umekuwa ukitokea katika eneo hilo.

Michuano hiyo mwaka huu ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa Manyara,Makongoro Nyerere ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa mkoa,Carolina Mtakula.

Akizundua michuano hiyo alitaka vijana wa Burunge kuwa mabalozi wa kupiga vita ujangili wa katika vijiji vyao.

mwisho.