Site icon A24TV News

NABII GEOR DAVIE AGAWA BAJAJI KWA VIJANA WABADILISHA MAISHA TUMEJENGA NYUMBA NZURI

Na Geofrey Stephen Arusha

Kiongozi mkuu wa huduma ya Ngurumo ya upako yenye makao makuu jijini Arusha,Mh Dkt Nabii Geor Davie ameendelea kuwa baraka kwa wahitaji wenye mahitaji ya kimwili pamoja na kiroho kwa kuwapa vijana bajaji na piki piki .

Aidha Nabii Dkt Geor Davie amekuwa mwangaza hata kwa taasisi za Serikali kwa kuwa amejijengea tabia ya kuwasaidia kwenye maitaji mbalimbali wakiwemo Askari Magereza .

Wakizungumza na Arusha 24Tv Vijana waliopewa Bajaji  na kusema kwamba kwa sasa wamefanikiwa katika Maisha kwani Nabii Dkt Geor Davie.amekua Msaada kwa Vijana na kina Mama jambo ambalo ni baraka sana kwao .

“Baba amekuwa ni msaada mkubwa sana hasa kwa jamii ambazo zinawaitaji,ukiangalia hata upande wa wasanii nao wamepewa misaada na mpaka wengine wamepewa magari kabisa

Wapo wasanii ambao wanamtumikoa Mungu tena kwenye mazingira magumu hawana mtu wa kuwasaidia lakini baba Dkt Geor Davie amekuwa akiwaona,mwaka jana msanii Good luck Hozbert alipewa gari,na kama haitoshi ametoa tena kwa msanii ajulikanaye kama Mkaliwao na wote tukiangalia namna ambavyo vijana hao wanamtukuza Mungu “waliongeza

Vijana hao kwa pamoja wamemshukuru Nabii Mkuu Geor Davie kwa Msaada huo wa bajaji na wamesema familia zao zimekua na Maisha Mazuri kwani hapo awali walikua wanaendesha bajaji za mkopo ambazo wasipofikisha maesabu wanalazimika kunyanganywa na maboss wao

Aidha wamesema kwamba mpaka sasa wamenunua Viwanja vya kujenga nyumba za kuoshi na familia zao hulu pesa zingine wakianzisha miradi mbali mbali kwa lengo la kujikwamua kimaisha

Baraka David na Elirehema Wamesema kwamba likubwa wanacho jivunia kutoka kwa Nabiii Geo Davie ni kwamba angalii mtu wa kumsaidia bali yeyote atakaye kua na uwitaji anamtia moyo na kumshika mkono huku akiwapa maneno ya faraja kwamba waongeze bidii katika kujituma kufanya kazi na kuondokana na umaskini

Mwisho