Site icon A24TV News

PSSSF KULIPA SHILINGI BILION 20 WATUMISHI WA VYETI FEKI

Na Doreen Aloyce,Dodoma

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF umesema unatarajia kuanza kuwalipa Watumishi waliokutwa na Vyeti Feki Jumla ya Shilingi Bilioni 20 ndani ya siku60takribani watumishi9000 mara baada tu yakupokea madai yao kutoka kwa waliyokuwa Waajiri wao.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo,ACP Hosea Kashimba ameyaeleza hayo Leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa PSSSF na mwelekeo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.

ACP Kashimba amebainisha kuwa hadi kufikia Mwezi Juni Mwaka2022Mfuko huo ulikuwa na Uwekezaji wenye thamani ya Shilingi Trlioni 7.5kwaajili ya kufanya uendelevu wa Mfuko huo.

 

“Mafao yaliyotolewa na mifuko ya pensheni ambapo kuanzia Julai 1,mwaka huu wanachama wote wa mifuko ya pensheni wanalipwa mafao ya uzee kwa kutumia kanuni zinazofanana ambazo zinalipa mafao bora na kuwezesha mifuko,”amesema CPA Hosea.

Pamoja na hayo CPA Kashimba ameeleza kuwa Mfuko huo unatambua Moja ya changamoto kubwa kwenye jamii ni uelewa mdogo kuhusu sekta ya hifadhi ya jamii hivyo PSSSF imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wanachama wake ili kuhakikisha sekta hiyo inafanikiwa .

Amesema kuwa ili jitihada za kuhakikisha lengo la kutoa huduma bora linatimia,Mfuko unaendelea kutekeleza mambo mbalimbali yanayolenga kurahisisha utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na mtandao wa Ofisi za Mfuko ambapo una Ofisi Kila Mkoa na baadhi ya Wilaya Kwa lengo la kuwa karibu na wanachama.

“Mfuko una kituo cha kupiga simu bure kwa ajiri ya wanachama ambapo huduma hutolewa hadi saa mbili usiku ikiwemo mfumo wa ufuatiliaji wa masuala ya yanayohusu huduma mbalimbali za uanachama,”amesema CPA Kashimba.

Akieleza matarajio ya baadae,amesema wanatarajia kuongeza vituo vya uhakiki Katika halmashauri mbalimbali na kuanzisha utaratibu wa kujihakiki kupitia simu janja na kusaidia Kila taarifa ya mwanachama iwe kwenye mfumo.

“Matarajio mengine ni kuhakikisha mifumo ya PSSSF inasomana na mifumo mingine kutoka Taasisi za Umma zinazotoa huduma,kurahisisha uandikishaji wanachama na uletaji wa madai kupitia mtandao na kutumia mifumo mipya ya Tehama kulingana na mahitaji ya Mfuko,”amesema

CPA Hosea ametaja matarajio mengine kuwa ni kubuni mifumo mipya na salama ya TEHAMA kulingana na mahitaji ya mfuko pamoja na kutumia mifumo ya TEHAMA kwa asilimia 85 huku lengo likiwa ni kutumia kwa asilimia 100 ifikapo 2023 katika shughuli za Mfuko hivyo kuboresha utoaji huduma.

Ikumbukwe kuwa mfuko wa PSSSF ulianzishwa mwaka 2018 kupitia sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma Namba 2 ya mwaka 2018 ambapo mfuko huo ni matokeo ya kuunganishwa kwa iliyokuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ya GEPF (1942),LAPF (1944),PPF (1978) na PSPF(1999).

 

Mwisho.