Site icon A24TV News

Shirika la Women and Children Welfare Support Kujibu Maombi ya Kupinga Ndoa Umri Miaka 15

Na Mwandishi wa A24Tv .

Taharifa kwa wananchi Tunapenda kuwajulisha kwamba SHAURI (kesi) ya Kikatiba Namba 14 ya mwaka 2022 iliyofunguliwa na MARY BARNABA MUSHI wa Shirika la Women and Children Welfare Support katika Mahakama Kuu Masijala Kuu ya Dar es Salaam dhidi ya Wakili Mkuu wa Serikali kupinga mchakato wa kukusanya maoni kuhusu MABORESHO YA SHERIA YA NDOA ,uliotangazwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dk Damas Daniel Ndumbaro (MB) imetajwa leo Tarehe 09 November 2022 Mbele ya Muheshimiwa Jaji Mosses Gunga Mzuna ambapo waleta maombi wamepewa siku mbili (2) kuwasilisha maombi ya nyongeza (Rejoinder ) na Tarehe 15 Shauri litatajwa tena kwa ajili ya kupanga siku ya kusikizwa.

MAOMBI YETU KWA MAHAKAMA
Tunaomba Mahakama itoe TAMKO KWAMBA:
1: Umri wa chini wa kuolewa kwa mtoto wa kike ni miaka 18 na upo hakuna mkanganyiko kufuatia matokeo ya uamuzi wa Mwanasheria Mkuu dhidi ya Rebecca Gyumi [2019] TZCA 348.;

Kuanzia tarehe 07.06.2017, kifungu cha 13 na 17 cha Sheria ya Sheria ya ndoa ilikoma kuwa sehemu ya sheria za Tanzania. 

Kwa sasa Kifungu cha 13 na 17 si sehemu ya Sheria ya Ndoa na kujumuishwa kwao katika Toleo Lililorekebishwa la Sheria la 2019 kulikuwa jambo la kusikitisha na bila kukusudia.

Waziri wa Sheria na Katiba ana wajibu wa kikatiba kuheshimu na kutekeleza maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na Mahakama ya Tanzania bila ucheleweshaji usiostahili.

Kufuatia matokeo ya Hukumu ya Mahakama ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Rebecca Gyumi [2019] TZCA 348; mashauriano yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania kuhusu umri wa chini kabisa wa kuolewa hauendani na Kifungu cha 107A[1] na 107B cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo basi ni kinyume na katiba na ni batili.

Mashauriano yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania na kuzingatia umri wa chini wa kuolewa kunadhoofisha nafasi ya Mahakama kama mamlaka ya mwisho ya kutoa haki nchini Tanzania.

Mahakama itoe AMRI kusimamisha mashauriano yanayoendelea kuhusu umri wa chini ya mototo wa kike kuolewa kwa sababu yanadhoofisha jukumu; nafasi na hadhi ya Mahakama ya Tanzania.

Hivyo tunaomba Wananchi na Wanaharakati wa Haki za Binadamu na Haki za Kijinsia kujitokeza kuhudhuria Mahakamani kesho tarehe 09 November 2022 saa 3:00 Asubuhi mbele ya Mh Jaji M.Mzuna kesi itakapotajwa kwa mara ya pilli .