Na Dorice Aloyce
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeleza kuwa uwepo wa vivutio vizuri na vya kipekee vya Utalii katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania ni fursa kwa wananchi wa mikoa hiyo kuendelea kunufaika kiuchumi kutokana na shughuli za utalii zinazofanyika.
Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo leo Novemba 10, 2022 mkoani Iringa alipokuwa akifungua rasmi Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka katika mikoa kumi ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Songwe, Rukwa na Katavi.
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa Utalii waendelee kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Hifadhi ya Taifa Nyerere ambayo ni kubwa kuliko zote Tanzania na Afrika ,Hifadhi za Taifa Ruaha, Mikumi, Udzungwa, Kitulo na Katavi.
Pia amesema mikoa hiyo imebarikiwa kuwa na Mapori ya Akiba ya Mpanga Kipengere na Selous, maeneo ya fukwe za Bahari ya Hindi na hifadhi zilizoko Lindi na Mtwara, Fukwe za Ziwa Nyasa na Tanganyika, Hifadhi za Misitu ya Mazingira Asilia Ziwa Ngosi na Hifadhi ya Asili Kilombero.
Aidha, amebainisha kuwa mikoa hiyo ina Maporomoko ya maji yanayovutia kwa shughuli za utalii kama Kalambo ambayo ni marefu Afrika, maeneo ya kihistoria, Kimondo cha Mbozi, Magofu ya Kale na ya Kilwa Kisiwani, Songo Mnara na Mji Mkongwe wa Mikindani ,utalii wa utamaduni wa mila na desturi na kazi za sanaa za mikono.
Sanjari na hayo pia Mhe.Dkt.Chana amesema kuwa Tanznia ni miongoni mwa nchi ambazo zinaongoza kuwa ya kwanza Dunia kuwa na wanyama aina ya Nyati hiyo ni kutokana na Mamlaka zinazosimia maeneo ya hifadhi kukabiliana kikamilifu na majangili.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeleza kuwa uwepo wa vivutio vizuri na vya kipekee vya Utalii katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania ni fursa kwa wananchi wa mikoa hiyo kuendelea kunufaika kiuchumi kutokana na shughuli za utalii zinazofanyika.
Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo leo Novemba 09, 2022 mkoani Iringa alipokuwa akifungua rasmi Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka katika mikoa kumi ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Songwe, Rukwa na Katavi.
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa Utalii waendelee kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Hifadhi ya Taifa Nyerere ambayo ni kubwa kuliko zote Tanzania na Afrika ,Hifadhi za Taifa Ruaha, Mikumi, Udzungwa, Kitulo na Katavi.
Pia amesema mikoa hiyo imebarikiwa kuwa na Mapori ya Akiba ya Mpanga Kipengere na Selous, maeneo ya fukwe za Bahari ya Hindi na hifadhi zilizoko Lindi na Mtwara, Fukwe za Ziwa Nyasa na Tanganyika, Hifadhi za Misitu ya Mazingira Asilia Ziwa Ngosi na Hifadhi ya Asili Kilombero.
Aidha, amebainisha kuwa mikoa hiyo ina Maporomoko ya maji yanayovutia kwa shughuli za utalii kama Kalambo ambayo ni marefu Afrika, maeneo ya kihistoria, Kimondo cha Mbozi, Magofu ya Kale na ya Kilwa Kisiwani, Songo Mnara na Mji Mkongwe wa Mikindani ,utalii wa utamaduni wa mila na desturi na kazi za sanaa za mikono.
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesisitiza kuwa Kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza Utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour, imeleta neema ya ujio wa wageni wengi nchini ambapo hadi kufikia mwezi Septemba, 2022 idadi ya watalii ilikuwa 1,034,180.
Aidha, amesema jitihada zaidi zinahitajika kuimarisha miundombinu ya utalii, kupanua wigo wa mazao mapya ya utalii, kuboresha huduma na kuendelea kutangaza zaidi vivutio vya utalii ili kufikisha lengo la watalii milioni 5 na mapato Dola za Marekani bilioni 6 ifikapo mwaka 2025.