Site icon A24TV News

WAANDISHI ANDIKENI HABARI BUNIFU ZINAZOCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI

 NA: VERONICA MAKONGO, ARUSHA

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye manufaa Kwa jamii Kwa kuandika habari bunifu zinazolenga kuwakwamua wananchi  kuondokana janga la umaskini.

Sekta ya habari na utangazaji ikitumika ipasavyo hususani vyombo vya habari mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia  vinaharakisha  zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka  zaidi hivyo kuwa chachu ya mabadiliko

Mkurugenzi wa taasisi ya wanahabari ya MAIPAC  Bw Musa Juma akitoa hotuba katika mahafali ya 16 ya chuo cha uandishi wa habari Fanikiwa. PICHA na Marystela Bryson.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wanahabari inayosaidia jamii za pembezoni nchini MAIPAC, Bw Musa Juma wakati akihutubia wahitimu na wazazi katika mahafali ya 16 ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Fanikiwa Arusha yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS  jijini Arusha mapema leo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa ulimwengu wa sasa umekuwa, haswa  katika eneo la sayansi na teknolojia hvyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo wa teknolojia kwa kuandika habari Bora na bunifu pia kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo  vitawasaidia wao kujiajiri.

Wahitimu Wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazazji Fanikiwa AushaPICHA na Marystela Bryson

Hata hivyo ameeleza kuwa  waandishi wengi wanaweza kufungua “Blog, radio mtandao na  Tv za Mitandaoni ambazo  wanaweza kupeleka maudhui mbali mbali ya kihabari na kupitia vyombo hvyo watapatikana wawekezaji mbalimbali ambao wataweka matangazo ya biashara zao ili zionekane na watazamaji au pengine wasomaji.Musa Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi MISA – TAN na Mkuu wa magazeti ya mwananchii Mkoani Arusha amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habari za mazingira, kilimo, uchumi, na  mabadiliko ya TABIA NCHI ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.

Naye mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi  wa wahitimu hao  kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo.

Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Fanikiwa Bw Andrea Ngobole akitoa hotuba kwa wahitimu wa chuo hicho mapema leo. PICHA NA Marystela Bryson.

Aidha katika Mahafali Hayo wahitimu wapatao 40 wamehitimu mafunzo yao ya umahiri katika Tasnia ya habari na utangazaji ambapo pia wamedhamiria kwenda kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya habari na utangazaji.

Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja wakisikiliza Kwa makini hotuba ya mhgeni rasmi.