Site icon A24TV News

WAJAWAZITO WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI.

Na Mwandishi wa A24Tv

Wajawazito wametakiwa kuzingatia lishe bora inayoambatana na kufanya mazoezi wakati wote wa ujauzito ilibkulinda Afya ya mama na Mtoto.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Tameke Joketi Mwegelo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mtendaji wa kata ya Charambe Theodora Malata katika hafla ya kuelekea uzinduzi wa Temeke Maternal Jogging uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Zakhem wilayani Temeke ,Dar es Salaam ukiwa na lengo la kuihamasisha jamii kuhusiana na lishe bora wakati na baada ya ujauzito utakaosaidia kujenga kizazi bora.

DC Joketi kupitia kwa muwakilishi wake Theodora ameishukuru Kampuni ya Hatua Group Afrika inayoratibu program ya BUSELA kwa kuwapatia vifaa vinavyotumika wakati wa Kujifungua ” Delivery Kits” Mia mbili kwa Wajawazito zaidi ya Mia mbili huku akitoa wito Kwa wajawazito hao kuzingatia lishe bora na kuzingatia mazoezi hata baada ya kujifungua.

Programu ya BUSELA imekuwa ikitoa elimu ya Afya ya Uzazi,lishe Bora, mazoezi na kuwajenga kisaikolojia Wajawazito kabla na baada ya kujifungua lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi huku mpango huo ukiwa ni wa miaka mitano utakaofanyika mikoa yote nchini,uzinduzi rasmi wa Maternal Jogging utafanyika february 2023.