Site icon A24TV News

WALIOSHIKWA MKONO NA NABII MKUU GEOR DAVIE WAMSHUKURU WAMO VIONGOZI WA SERIKALI

Na Geofrey  Stephen  Arusha

Kiongozi mkuu wa huduma ya Ngurumo ya upako yenye makao makuu jijini Arusha,Dkt Nabii Geor Davie ameendelea kuwa baraka kwa wahitaji wenye mahitaji ya kimwili pamoja na kiroho kwa kuwapa mitaji

Aidha Nabii Dkt Geor Davie amekuwa mwangaza hata kwa taasisi za Serikali kwa kuwa amejijengea tabia ya kuwasaidia kwenye maitaji mbalimbali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na Mwandishi wa habari hizi waliofanikiwa kupewa mitaji na misaada kutoka Nabii Dkt Geor Davie walisema kuwa anafanya yale ambayo yameandikwa katika maandiko matakatifu

“Baba amekuwa ni msaada mkubwa sana hasa kwa jamii ambazo zinawaitaji,ukiangalia hata upande wa wasanii nao wamepewa misaada na mpaka wengine wamepewa magari kabisa

Wapo wasanii ambao wanamtumikoa Mungu tena kwenye mazingira magumu hawana mtu wa kuwasaidia lakini baba Dkt Geor Davie amekuwa akiwaona,mwaka jana msanii Good luck Hozbert alipewa gari,na kama haitoshi ametoa tena kwa msanii ajulikanaye kama Mkaliwao na wote tukiangalia namna ambavyo vijana hao wanamtukuza Mungu “waliongeza

Akiongea kwenye hafla kubwa sana ambayo ilifanyika katika mji wa daudi Kisongo Arusha wiki chache zilizopita Nabii mkuu Dkt Geor Davie alisema kuwa anazidi kutokomeza umaskini

alisema kuwa fedha ambazo amekuwa akizitoa ni kama mbegu kwa ajili ya kutokomeza umaskini

“Jamani kuna mtu ambaye nimempa Gari na anamtukuza Mungu,tuwasaidie watu ni mbegu tunapanda na ukifanya jambo ambalo ni Jema ni utukufu”aliongeza”.

Naye Balozi kutoka Ngurumo ya Upako Nabii Sekela ntondolo alisema kuwa ili usipitwe na baraka za Mungu ni lazima uhakikishe kuwa unafanya jambo Kwa Mungu

Nsekela alisema kuwa fursa zipo nyingi sana lakini wakati mwingine hazionekani kwa uraisi.

“Tunatakiwa tujifunze kutoka kwa baba yetu Nabii Dkt Geor Davie jinsi ambavyo amefanyika baraka”aliongeza

“Tunatakiwa kukataa udhaifu wa aina yoyote Ile na tuzidishe bidii na makanisa yetu ambayo yanaitaji kujengwa”aliongeza
Mwisho .