Site icon A24TV News

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

Na Doreen Aloyce, Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini lengo ni kuboresha mazingira ya ufundishaji Kwa njia ya TEHAMA.

Ameagiza vishikwambi hivyo kuwafikia walengwa pasipo ubadhilifu huku akiwasisitiza walimu kuvitumia kwa usahihi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Majaliwa amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa vitendo kuwekeza katika eneo la TEHAMA ili vijana wapate ajira na kujiajiri wenyewe kupitia shughuli mbalimbali na kusaidia Taifa kukua kiuchumi.

Amesema adhma hiyo inaakisi mpango mkakati wa maendeleo wa Taifa ambao unaainisha afua ya kimkakati katika kuboresha na kuimarisha utoaji wa elimu nchini ambapo moja ya maeneo ya kipaumbele ni kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kuboresha Maisha.

” Serikali ya awamu ya sita tangu kuingia madarakani imewekeza sana katika eneo laTEHAMA uwekezaji huo umeelekezwa katika maeneo ya miundombinu,vitendea kazi, mitaala na mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wetu hususan walimu ili kuboresha ufundishaji,usimwambie na ufuatiliaji,”amesema

Waziri Mkuu amesema pamoja na utekelezaji wa mpango huo kumekuwa na uhitaji wa vifaa vya TEHAMA katika shule hasa kwa walimu katika maandalizi ya ufundishaji,usimamizi na upimaji wa sekta ya elimu nchini.

Amesema serikali ya Rais Samia imeamua kununua vishikwambi Kwa ajili ya walimu na wakufunzi wote nchini waliopi katika shule za msingi,sekondari ,vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi na mafunzo ya mafundi stadi,vyuo vya maendeleo ya wananchi na wadhibiti ubora WA shule.

“Tunapo gawa vishikwambi Leo nataka nitoe maelekezo kwa Mamlaka zote zinazohusika katika zoezi hili kuhakikisha vifaa hivyo vinawafikia walimu wote kwa wakati ili vifanye kazi iliyokusudiwa.

Ameongeza kuwa “Hapa napendabkusisitiza kuwa vishikwambi hivi ni kwa ajili ya walimu tu na sio maofisa wa sekta nyingine au viongozi wa kisasa hivyo wanaohusika wahakikishe hakuna mwalimu atakayekosa kishikwambi na idadi ya walimu tunayo .

Amesisitiza kuwa vishikwambi hivyo vitakuwa Mali ya mwali husika na atakayekosa atoe taarifa ili kufuatilia.

MAELEKEZO.

Waziri Mkuu ametoa tisa kwa mamlaka zinazohusika ikiwemo kuhakikisha vifaa hivyo vinawafikia walenngwa kwa wakati pasipo ubadhilifu wowote.

Amesema pia viongozi wahakikishe kila mwalimu anapata kishikwambi.

“Nawaagiza walimu kuhakikisha vifaa hivi vinatumika kwa usahihi ili vikalete matokeo chanya katika sekta ya elimu na kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili kwenye ufundishaji,

Ameongeza kuwa”Kishikwambi aligawiwa mwalimu ni Mali yake husika hivyo viongozi wahakikishe wanaandaa mafunzo maalumu namna ya kutumia vifaa hivyo Kwa walimu.

Waziri Mkuu amewataka walimu kuvitunza vishikwambi hivyo kwa manufaa ya taifa ili kuimarisha kwa ufundishaji wa somo la TEHAMA.

WAZIRI MKENDA

Kwà upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa.Adolf Mkenda amesema kuwa katika jitihada za kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji nchini, Serikali kupitia Wizara hiyo imenunua jumla ya vishikwambi 300,000.

Ambapo mgawanyo wa Vishikwambi hivyo 6,600 vimekabidhiwa kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vishikwambi 293,400 vimebaki Tanzania Bara.

Prof.Mkenda amesema kuwa vishikwambi 293,400 vimegawiwa Kwa walimu wa shule za Msingi za umma wamekabidhiwa Vishikwambi 185,404,Walimu wa Shule za Sekondari Vishikwambi 89,805,Wathibitì Ubora wa Shule ngazi ya Wilaya na Kanda Vishikwambi 1,666, Wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu vya Umma,vishikwambi 1353,Wakufunzi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC) Vishikwambi 297.

Wengine waliyopatiwa Vishikwambi ni Maafisa Elimu ngazi ya Mkoa,Wilaya na kata ,vishikwambi 5,772,Wakufunzi wa Vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi-VETA vishikwambi 996 na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Vishikwambi 8,357.

Mwisho