Site icon A24TV News

Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki lazindua  mkakati wa miaka mitano wa kuwezesha wanawake viongozi. 

Geofrey Stephen , Arusha.

Arusha.Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Fatuma Ndangiza kutoka nchini Kigali Rwanda amesema  kuwa bunge hilo limezindua mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka 2022 mpaka 2027 ambao unalenga kuwapa viongozi wanawake namna ya kufuatilia maendeleo ya wanawake pamoja na kufuatilia fursa mbali mbali ambazo zinatokana na jumuiya ya Africa Mashariki .

Akizungumza na  waandishi wa habari Mbunge Fatuma amesema kuwa ,mkakati huo  utawasaidia wabunge wanawake kujieleza na kuuliza maswali ya maendeleo katika bunge hilo na kuweza kuboresha maswala mbalimbali yahusuyo  wanawake katika nchi hizo za jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema kuwa,kuzinduliwa kwa mkakati huo ni sehemu mojawapo ya kuendelea kusonga mbele kwa kuwapata viongozi wanawake katika nchi wanachama wa jumuiya ya Africa Mashariki.

Ameongeza kuwa, katika bunge la nne wamejitahidi kufanya marekebisho makubwa katika katiba za jumuiya na nchi zao kuendelea kutoa kipaumbele  katika kuwapa wanawake nafazi mbalimbali za uongozi.

Aidha amesema kuwa , matarajio makubwa yanategemewa katika nchi wanachama kupitia bunge la tano ambalo limeanza hivi karibuni baada ya kupata wabunge wengi wanawake ambapo katika vikao vyao wataendelea kupigania usawa wa wanawake katika uongozi kwa nchi za jumuiya Afrika Mashariki ambapo  matarajio hayo yatafikiwa  hadi mwaka 2027.

“Tunajivunia kuona nchi ya Tanzania  kuna Rais Mwanamke pia tunajivunia nchi za Afrika Mashariki kuna wabunge mawaziri  wanawake pamoja na wengine ambao kati yao saba ni wanawake lakini pia nchini Ruanda kuna viongozi wanawake ambao ni asilimia hamsini wakiwa wanawake ambao ni wakuu wa mikoa na sekta binafsi ambapo  sheria hizo  zimewekwa  katika nchi za jumuiya ya Africa Mashariki .”amesema Fatuma.

Mwisho.