Site icon A24TV News

DC NJOMBE:WANAFUNZI KUNUNULIWA GARI NA KUPANGISHIWA NYUMBA NA WANAUME NAO NI UKATILI WA KIJINSIA

Na Mwandishi wa A24Tv .

Wakati Tanzania ikiendelea kupinga ukatili wa Kijinsia kupitia siku 16 za kabilibiana na janga hilo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema hata vitendo vinavyofanywa kwa wanafunzi mbalimbali ikiwemo kuwanunulia simu,gari na hata kuwapangishia nyumba ni ukatili pia unaopaswa kupigwa vita.

Katika mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika @wildaftz kupitia mradi wa mwanamke Imara ukihusisha wanafunzo wa vyuo vikuu na vyuo vya kati takribani sita Kasongwa amesema ipo haja ya kuongeza nguvu katika kupinga ukatili huo kwa wanafunzi na watoto nchini.

Aidha Kasongwa amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuendelea kutangaza habari za ukatili kwa nguvu na hatua zinazochukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo.

Hata hivyo ameonesha masikitiko makubwa juu ya kuwapo kwa baadhi ya wanaume wanaojiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja huku akitaka sheria zichukua mkondo wake dhidi ya watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Susan Kawanga ni Mratibu wa mradi wa Mwanamke Imara toka shirika la Wildaf ambaye amesema wameandaa mdahalo huo katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ukiwa na lengo la kutaka kujadili changamoto zilizopo vyuoni hususani rushwa za ngono na ukatili mwingine.